Adverts

Feb 6, 2011

Hili la Diwani mpya wa TLP Arusha laweza kuanzisha tena ghasia kubwa

Hili la Diwani mpya wa TLP Arusha laweza kuanzisha tena ghasia kubwa: "
TLP wapinga NEC kuwateuliwa diwani Sakata la umeya wa Manispaa ya Arusha inazidi kuchukua sura mpya baada ya Chama cha Tanzania Labour (TLP) kupinga uamuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupitisha uteuzi wa Mwaija Choga kuwa Diwani Viti Maalum kupitia chama hicho mkoani Arusha, kikidai kuwa si mwanachama wake halali. Hatua hiyo imefuatia baada ya uongozi wa chama hicho mkoani hapa ukiujulisha uteuzi huo na kuagiza kumuarifu diwani huyo taratibu za kuapishwa kabla ya kuanza kutekeleza majukumu. “Napenda kukutaarifu kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemteua Mwaija Choga kuwa Diwaninwa Viti Maalum katika Halmashauri ya manispaa ya Arusha, kwa barua ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Kumb Na. EA.47/74/01/26 ya January 27, 2011” inaeleza sehemu ya barua ya kutoka kwa mkurugenzi wa Halamashauri ambayo Mwananchi Jumapili imeiona…….. ………..Mwenyekiti wa TLP mkoani Arusha, Leonard makanzo, alisema jana kuwa TLP imepinga kwa nguvu zote uteuzi huo kwa maelezo Choga si mwanachama wa chama hicho, kuanzia Novemba 16, 2010. “Choga hawezi kutambuliwa kama Diwani wa Viti Maalum kupitia chama hicho cha na hastahili kutambuliwa kuwa diwani na asihudhurie vikao vyovyote vya baraza la madiwani vya halmashauri hiyo kwa tiketi ya TLP,” alisema Makanzo…. Naye Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema uteuzi wa diwani huyo haukufuata taratibu na kwamba jina la Chogga halikuwa pendekezo la Kamati Kuu ya TLP Taifa. Mrema alisema maofisa watatu ndani ya chama hicho wakishirikiana na Chogga walifanya njama kuhujumu jina halali la mgombea lililopelekwa NEC……. Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili. .
"