Kuna tatizo sugu ambalo linawakabili watu wengi (hususan wanaume). Hata kama inatokea kwa wanawake lakini maumbile yao yanawabeba.
Ni tatizo la kuzidiwa na hisia ambalo matokeo yake ni aibu. Kijana kumpata mama, katika safari faragha kujikuta ametia nanga kabla mashua haijang’oka.
Aghalabu, mtu anapojifunga goli mwenyewe kabla ya mechi, huona aibu. Matokeo yake hata achangamshwe na apewe muda vipi, hushindwa kurudi mchezoni.
Kinachowauma vijana au hata wanaume watu wazima wengi ni lile swali la “imekuwaje tena?” Hilo huulizwa na mwanamke baada ya kuona mchezaji anahangaika badala ya kuingia uwanjani. Kisaikolojia, swali hilo huyeyusha hisia zote ndani ya ubongo. Kinachofuata badala ya kutuliza akili ili ajipange, muda mwingi huutumia kutafakari aibu aliyoipata. Mawazo yake huenda mbali zaidi na kuanza kuhisi ni mgonjwa. Matokeo yake hata akikaribishwa uwanjani na mtu huyo huyo siku ya pili, hushindwa kwa sababu ya wasiwasi. Akidhani la jana litajirudia. CHANZO CHA TATIZO Kuna mambo makuu matatu ambayo kwa namna moja au nyingine husababisha hali hiyo itokee, lakini moja linaweza kuzaa lingine. MOSI: WASIWASI (WOGA) Mwanamke anapokabiliwa na wasiwasi, maana yake mwili wake hauwezi kuwa tayari kwa tendo. Atabaki mkavu, mwanaume ambaye atalazimisha, atamuumiza kwa kumchanachana kama si kumchubua. Tofauti ni kwamba mwanaume akiwa na wasiwasi, husinyaa. Kichwa chake kitakabiliwa na mawazo mengi ambayo mwisho humfanya ashindwe kumudu kitu chochote. Kuna woga wa aina mbili. Wa kwanza ni ule wa kumwogopa mwanamke kwa sababu mbalimbali. Umri, umbile, pengine kuna tishio kuwa huyo ni mali ya mwingine au umeambiwa ana maradhi. Hofu hiyo inaweza kukufanya ushindwe kusukuma ‘ligwaride’, hivyo utabaki umesinyaa. Woga wa pili ni ule wa kuona mtu yupo mbele yako lakini ukaanza kumwogopa. Kilichopo ni kuwa unamtafakari kwa chati, pengine mwonekano wake unakumaliza haraka. Hisia zinakuwa juu, kiasi kwamba anapokufungulia uwanja ili uingie, unajikuta unafunga goli uwanjani. Huu ndiyo woga ambao namaanisha. Kwa maana unajitikisia nyavu mwenyewe. Unabaki na aibu ambayo hukupeleka kwenye hisia za kwamba unaumwa. Nifafanue kitu hapa kuwa tabia ya kuogopa ‘ukubwa wa samaki’ ndiyo huwafanya wengi wapatwe na hali hii. Kwamba, alipokuwa anamwona mtaani hakuamini kama kuna siku yangetimia. PILI: PUPA Katika pointi hii ni kuwa kuna watu wakishatongoza au kumwona tu mwanamke barabarani na kumpenda, kuanzia nukta hiyo akili zao huharibika. Akilala humuota mwanamke huyo, akikaa peke yake mawazo yake yote huelekea kwa mrembo husika. Hali hiyo husababisha kuupa mwili mzigo mkubwa wa hisia. Mwingine hufika mbali zaidi, kwani huwaza mpaka akiwa chumbani na mwanamke husika, akimtafakari bila wazo lolote mwilini na jinsi atakavyomkabili. Hulka hiyo husababisha wengi kujichafua ndotoni. Lakini hiyo siyo hasara pekee, kwani kubwa zaidi ni ile ya kujikuta ukiwa na hali ya “siamini macho yangu” pale utakapofanikiwa kumpata kweli. Umeshamuwaza sana, umemuota mara nyingi, mwili ukawa unapandwa na joto ukiwa peke yako, matokeo siku ya tukio unakuwa na pupa, hivyo kujikuta unachana nyavu ukiwa nje ya uwanja. Mkamia maji hayanywi! Ukishapatwa na hali hiyo, hutaweza tena kurudi uwanjani, kwa sababu akili yako itaingiwa na woga uliotokana na aibu kwa kuona kwamba mrembo atakuona huwezi kazi. TATU: KUJIONA WA CHINI Kinachobeba mantiki ya pointi hii ni kile cha kuogopa ukubwa wa samaki. Kuna mwanafasihi mmoja aliwahi kuimba: “Usiogope ukubwa wa samaki, uliza bei.” Watu wengine wanapoona warembo wazuri barabarani, hujiangalia kwanza wao na kujitoa kasoro kwa kujiona wapo kiwango cha chini. Hali hiyo husababisha hata pale anapompata, ushindwe kufanya vizuri mchezo kwa ama kufungia nje au kuwahi mapema kwa sababu ya kuzidiwa na hisia za kutoamini macho yako kama umempata. NNE: KUTOSHIRIKI TENDO KWA MUDA MREFU Hili kwa wengine huweza kuwa tatizo. Umekaa muda mrefu bila kufanya kweli, mzigo unakuwa mwingi matokeo yake siku ya tukio unamwagika bila hodi. Kinachotakiwa hapo ni mtu kuelewa hali hiyo lakini kinyume chake huanza kujipa mawazo kwamba ameaibika na hawezi kazi, matokeo yake hushindwa kabisa. Huyo hata akiitwa kesho, atarudia yale yale. Kumbukumbu za jana zitaendelea kumuathiri na kusababisha aanze kujihisi ni mgonjwa na hana nguvu sahihi. Itaendelea wiki ijayo.