Adverts

Feb 14, 2011

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MTERA LEO.

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MTERA LEO.: "
Basi lililopakia wajumbe ya Kamati ya Nishati na Madini likipita katika eneo la Mlowa barabarani Mkoa wa Dodoma wakielekea kutembelea kituo cha kuzalisha umeme Mtera leo 13 Feb, 2011 (Picha na Dada Mwanakombo Jumaa wa Maelezo Dare salaam). Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na Mwenyekiti wa Kamati Bunge ya Nishati na Madini Januari Mkamba wakibadilishana mawazo wakati wakitembelea leo Bwawa la Mtera kuangalia hali ya upatikanaji wa umeme nchini.
Meneja Tanesco Mtera Justus Mtolera (kulia koti jeusi )akitoa maelezo ya hali ya upatikanaji wa umeme nchini. (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akifuatiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini January Makamba.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiangalia maji yaliofurika katika eneo la Mlowa barabarani mkoani Dodoma wakati wakielekea Bwawa la Mtera kuangalia hali ya upatikanaji umeme nchini leo.
"