Adverts

Feb 21, 2011

KARIBUNI UWANJI

SAFARINI MATAMBA Jana siku Kuu ya Maulid mimi na waminifu wangu tuliona tukaisherehekee kijiji cha Matamba wilayani Makete. Sio mbali sana na Mbeya Mjini. Ukiwa unaelekea Iringa unachepukia Chimala kuelekea milimani. Ni Milima iliyo mikali huwezi kudhani kuna hata barabara huko Hapa ni katikati ya safari yetu. Chini kule chini ndio mji wa Chimala. Hatuko kwenye ndege ama helikopta. Kwa mbali unaweza kuona barabara iendayo katika mashamba ya mpunga ya usangu. Pia unaweza kuona mashamba ya mpunga. Ukifika Matamba shurti upozee koo. Ulanzi huo. So sweeet. Ukiwa Matamba unakuwa karibu kabisa na vivutio vya kitalii kama ziwa Ngozi na Hifadhi ya taifa ya Kitulo. Huko tutafika siku zingine HUYU NI MWAIPOPO BLOG
"