Adverts

Feb 18, 2011

Kwa nini wanandoa wasiopata mtoto lawama huelekezwa kwanza kwa mwanamke??

swali!!!!!
Kuna tabia imejengeka tangu enzi na enzi ya kuelekeza lawama kwa mwanamke pindi ndoa inapokosa mtoto. Mbaya zaidi, mwanamke ndiye anayesukumwa aende hospitali kupimwa. Halafu hata akipimwa na kuonekana hana matatizo mwanaume anakuwa mgumu kupimwa ana lawama zinaendelea kuelekezwa kwa mwanamke. Kwa maeneo mengine, mwanamke ndiye anayekuwa mhanga wa hilo tatizo hata kama wakati mwingine siyo yeye aliyesababisha. Hivi ni kwa nini tabia hii imeshamiri kiasi hicho? Kwa nini wanaume wengi hawapo tayari kupimwa, kama ilivyo kwa wanawake?
" mjadala kutoka Jamii forums