Adverts

Feb 8, 2011

Mwizi wa kuku

Mwizi wa kuku: "
Kuna mwizi mmoja alibahatika kuiba kuku lkn kuna jamaa wawili walikuwa wakimshuhudia ktk pilika zake hizo za kuiba na kuanza kumkimbiza,lkn wao walikuwa wanamkimbiza kimya kimya bila kupiga kelele za kumwita mwizi,ndipo yule mwizi akajua kwamba hawa jamaa watakuwa sio watu wema kwanini hawapigi kelele za mwizi! Ndipo yule mwizi akaamua kumchinja yule kuku na damu kujipaka ktk shati lake na kumchukua yule kuku kumuweka kwenye tumbo lake na kumchomoa kisu kwa juu ili mtu akipita aone kana kwamba amepigwa kisu cha tumbo na kulala chali kama amekufa,ghafla wale jamaa wakatokea na kumkuta mwizi ana kisu tumboni na wao wakaanza kujadiliana JAMAA#1:hii ujue kesi,watu wametuona tunavyomkimbiza huyu mwizi?kwahiyo madhali amekufa ujue lazima cc ndio tutakaoenda jela sasa tufanyeje? JAMAA#2:Mimi naona tukamtupe baharini Basi yule mwizi kusikia akatupwe baharini akaamka na kuanza kuhamaki MWIZI:Mizee mengine ina roho mbaya kweli wewe kuiba kuku tu mnataka mkanitupe baharini,je ningeiba ng'ombe mngenifanya nini?
"