Adverts

Feb 7, 2011

NYOSH EL SAADAT KAMA BOB MARLEY VILE

NYOSH EL SAADAT KAMA BOB MARLEY VILE: " Wiki ya mwisho wa mwezi wa kwanza nilifanya mahojiano na Nyoshi el saadat raisi wa vijana.Kiongozi wa band ya fm academia (wazee wa ngasuma) Tuliongea mengi sana...aliniambia baada ya miaka miwili kupita baada ya kifo cha mkewe Rukia Bruno itamchukua muda kuoa mwanamke mwingine maana Rukia alikuwa so special.Alichokuwa anapenda kwa Rukia alikuwa mtu watu,mcheshi...pia zile fujo na ugomvi kati yao ilikuwa ni chachu katika mapenzi yao.Hivyo imekuwa ngumu kumpata mwanamke wa hivyo na ameamua kukaa bila mahusiano na kulea watoto wake. Nyosh aliniambia ana watoto 6 na wote amewapata kwa wanawake 6 tofauti.Nikamuuliza hajisikii vibaya kuzaa na wanawake wote hao tena watoto ambao wanahitaji matunzo??akanijibu hiyo inaonyesha ni jinsi gani ana wapenzi wengi,anakubalika mpaka wanawake hao kutaka kuzaa na yeye. Hii naifananisha na ya hayati Bob Marley ambae ana watoto kibao kwa wanawake tofautitofauti na alinukuliwa akisema kuwa aliingia kwenye uhusiano na wanawake wengi kwa sababu ya kuwaonea huruma wanawake waliokuwa wakimpenda.Duniani kote alikokuwa akisafiri wanawake walikuwa wakimlilia na kuonyesha wanampenda na yeye hakuwa mchoyo kwao!!
"