Hawa ni askari wa kike Temeke jijini Dar es Salaam wakiwa na silaha ,ila polisi Iringa inasema askari wa kike hawana ruhusa ya kubeba silaha swali kwa jeshi la Polisi Iringa utaratibu huo ni Iringa pekee ama nchi nzima?mpendwa mdao japo napenda kuweka wazi kuwa hivi sasa jeshi la polisi Iringa limepata kunieleza wazi kuwa taarifa hii itanigharim hivyo binafsi nipo tayari kwa lolote Mungu ndiye muweza wa yote
Mtoto huyo aeleza alivyoshuhudia mama yake akipigwa risasi
"
Maelezo ya awali ya Hospitali ya mkoa wa Iringa dhidi ya mgonjwa huyo haya hapa ,japo zipo tetesi kuwa jeshi la polisi linafanya mkakati wa kubadili maelezo ya awali ili jumatatu kutoa taarifa za uchunguzi kwa vyombo vya habari.
Hata hivyo jana jeshi la polisi lilipata kumchukua mwanamke huyo na kumhoji zaidi juu ya tukio hilo baada ya mwanamke huyo Frida Mgimwa kwenda ofisini kwa mkuu wa wilaya ya Iringa kulalamikia suala hilo la kupigwa risasi na askari bila kutendewa haki na jeshi la polisi.