Adverts

Feb 6, 2011

Uwanja wa fainali ya kombe la Dunia wachakachuliwa

Uwanja wa fainali ya kombe la Dunia wachakachuliwa: "

Johannesburg, Soccer City, ambako mechi ya fainali ya kombe la dunia kwa mwaka 2010, ilifanyika

Vibaka nchini Afrika ya Kusini, wameiba nyaya za umeme na kuharibu mfumo wa umeme katika moja ya viwanja vilivyotumika wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010, zilizofanyika nchini humo.

Johannesburg, Soccer City Stadium, ambako mechi nane za kombe la dunia zilichezwa, ulikuwa utumike mwishoni nwa wiki kwa ajili ya pambano Kaizer Chiefs na Moroka Swallows, pambano ambalo limelazimika kuahirishwa kutokana na hitilafu hizo.

"