Adverts

Feb 2, 2011

UZINDUZI WA SHEREHE ZA KUZALIWA KWA CCM WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.

UZINDUZI WA SHEREHE ZA KUZALIWA KWA CCM WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.: "
Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzbar na makamu mwenyekiti wa CCM Zanzbar Dkt. Aman Abeid Karume akivalishwa skafu na vijana Chipukizi wa CCM mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Biafra jana jioni jijini Dar es salaam kuhudhuria Uzinduzi wa Sherehe za Kuzaliwa kwa CCM.

Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Picha no 7. Wanawake wa UWT mkoa wa Dar es salaam wakicheza muziki wakati wa Uzinduzi wa Sherehe za kuzaliwa kwa CCM jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzbar na makamu mwenyekiti wa CCM Zanzbar Dkt. Aman Abeid Karume, Katibu Mkuu wa CCM taifa Yusufu Makamba na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa kuangalia gwaride rasmi liloandaliwa na UVCCM wakati wa Uzinduzi wa sherehe za kuzaliwa kwa chama hicho jana jioni jijini Dar es salaam.

Kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara akiwachekesha wana CCM waliohudhuria kwenye sherehe za uzinduzi wa CCM kutimiza miaka 34 jana katika viwanja vya Biafra.
"