Adverts

Feb 19, 2011

Viongozi wa BAVICHA kujulikana Aprili

MKUTANO mkuu wa kuwachagua viongozi wa ngazi za juu wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) unatarajia kufanyika mwishoni mwa Aprili, mwaka huu. BAVICHA haina uongozi rasmi wa ngazi za juu baada ya uchaguzi wa baraza hilo kuharibika mwaka jana, kutokana na kasoro mbalimbali, hivyo nafasi hizo kuongozwa na Kamati ya Uendeshaji. Akizungumza na Tanzania Daima, Katibu Mkuu wa Kamati ya Uendeshaji, Ally Chitanda alisema tayari Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoketi Januari 29 na 30 mwaka huu, imebariki kufanyika kwa uchaguzi huo. Chitanda alisema kutokana na baraka hizo, kinachosubiriwa sasa ni maelekezo kutoka ngazi za juu za chama ili waweze kuanza maandalizi ya kufanikisha uchaguzi huo ikiwamo na kuwatangazia wajumbe na vijana wa chama hizo. “Kwa kuwa BAVICHA tutakuwa tunafanya uchaguzi wa kwanza ndani ya katiba mpya ya chama chetu …matumaini yangu uchaguzi utafanyika vizuri na tutapata viongozi wachapakazi kama ilivyo katika chama,” alisema Chitanda. Mkutano mkuu wa uchaguzi huo utaowajumlisha wajumbe kutoka katika majimbo na wilaya, utamchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti, wajumbe watano watakaoingia katika baraza kuu la chama na wajumbe 20 wa mkutano mkuu wa chama. My take: Siyo siri chama chochote cha siasa (modern political party) vijana huwa ndiyo moyo(engine) wa chama wanategemewa kwa mambo mengi hasa kwenye uhamasishaji. Natoa wito kwa Chadema wasiichezee tena hii nafasi, wakipoteza watakuwa wanachelewesha maendeleo ya chama, wanachama na wananchi wanaowategemea ajue kwamba mwaka 2015 si mbali kama wanavyofikiri.
"