Mhanga
"
Mkurugenzi wa Mahusiano na Vodacom Foundation Bi Mwamvita Makamba ameviambia vyombo vya habari kwamba.
Kampuni yake kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation umeguswa na janga la milipuko ya mabomu yaliyotokea katika kambi ya Jeshi Gongolamboto Jijini Dares Salaam
:Na hivyo kumfanya kuamua maamuzi ya haraka kama yafuatayo.1. Kufungua tena namba yao ya maafa ili kuruhusu watanzania ambao wangependa kuchangia wenzao kufanya hivyo kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15599 kupitia mitandao yote.Ujumbe huu utatozwa shilingi 1000 na pesa zote zitaenda kwenye tume ya maafa ya serikali ili kuweza kununua vitu vya dharura vya wahanga.
Red alert itawasha rasmi kesho ijumaa tarehe 18.2. Vodacom Foundation itatoa chakula na vinywaji kwa siku nzima ya ijumaa kwa wahanga zaidi ya 1000 waliopo Uwanja wa taifa ambao wengi wao ni watoto3.
Pia Vodacom foundation imetoa namba za simu kwa timu ya clouds ilioanzisha kituo cha habari na matukio huko shule ya mzambarauni ukonga.
Namba hizi zinatumika kupiga bure na kutoa taarifa ya kupotelewa Ndugu au jamaa na pia kutoa taarifa ya maafa zaidi ambayo hayajulikani ili taarifa ziende kwa wahusika.
Namba hizi ni 0767 111401 , 0767111402 na 07671114034. Pamoja na kuwawezesha watanzania kutuma mchango wao kupitia ujumbe mfupi, Vodacom Foundation pia unakusanya misaada ya chakula na maji na vifaa mbalimbali katika Ofisi zao zilizopo Mlimani city kwa watu ambao hawajui waipeleke wapi.
Misaada hiyo itakabidhiwa kwa red Cross ambao wanahudumia wahanga waliopo Uwanja wa taifa na sehemu mbalimbali