Adverts

Feb 9, 2011

Waziri auawa katika taifa jipya la Sudan ya Kusini

Waziri auawa katika taifa jipya la Sudan ya Kusini: "
Jimmy Lemi Milla (Photo: Government of Southern Sudan)

Jimmy Lemi Milla, ambaye ameuawa pamoja na bodi gadi wake

Inavyoonekana, kura ya maoni ya kuamua nchi ya Sudan kugawanyika na kuwa mataifa mawili, kwa maana ya Sudan ya Kaskazini na ile ya Kusini, bado haiwezi kuwa suluhisho baada ya kuuawa kwa mmoja wa mawaziri wa serikali ya Sudan ya Kusini, ikiwa ni siku chache sana toka kupigwa kwa kura ambayo ilionyesha kuwa sehemu hiyo ya Sudan, inataka kuwa taifa lenye kujitegemea.

Jimmy Lemi Milla, aliyekuwa waziri wa ushirika na maendeleo vijijini, aliuawa jana na aliyekuwa mfanyakazi wake wa zamani, ambaye pia alimuua na mlinzi wa waziri huyo, kabla ya muuaji mwenyewe kutiwa mbaroni, na hali hii imezua maswali miongoni mwa wanaofuatilia hatma ya Sudan kwa ujumla.

Muuaji huyo ambaye alikuwa ni sehemu ya wapiganaji wa SPLA, bado hajahojiwa juu ya sababu zilizomsukuma kufanya mauaji hayo, lakini viongozi wa ngazi za juu wa SPAL, wanaamini kuwa mauaji hayo yametokana na sababu binafsi zaidi badala ya itikadi za kisiasa.

Soma zaidi juu ya mkasa huu kwa kubonyeza hapa.

"