Baadhi ya waazee wakazi wa kijiji cha Kapele wilayani Mbozi wakitoa maelezo kwa mwandishi wa habari wa blog ya dtwevetz.blogspot juu ya jiko la kufua chuma lililo nyuma yao ambalo lilikuwa likitumiwa na mababu zao miaka 150 iliyopita. Jiko hili mpaka sasa lipo katika pori la kijiji hicho ambapo pia masalia ya chuma hupatikana hapo.
Mzee Sikanyika akionyesha kipande cha chuma kilichotolewa kwenye jiko la ufuaji chuma ambalo ni sehemu muhimu ya vivutio vya utalii wilayani mbozi.