Adverts

Mar 19, 2011

CUF YATAKA VIONGOZI WA CHADEMA WAKAMATWE KWA UHAINI..

"

CHAMA cha wananchi (CUF) kimewaasa watanzania kuepuka kushiriki maandamano ya yanayoendeshwa na viongozi wa kitaifa wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kuwa ni maandamano ya kichochezi yenye lengo la kuliingiza Taifa katika machafuko na kutaka serikali ya Rais Jakaya Kikwete kutofumbia macho kauli za kichochezi dhidi ya serikali .

Hata hivyo CUF imesema kuwa kinachofanywa na viongozi wa Chadema kwa kuhamasisha wananchi kutoiamini serikali iliyopo madarakani ni uhaini na viongozi wake wanapaswa kukamatwa na kufungwa jela kwa kosa la uhaini.

Kauli hiyo imetolewa leo katika uwanja wa Tangamano na mbunge wa jimbo la Wawi Zanzibar Hamad Rashid ambaye ni kiongozi kivuli wa wabunge wa CUF bungeni wakati akimkaribisha mweyekiti wa CUF Taifa Prof.Ibrahim Lipumba kuwahutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Tanga katika mkutano wa hadhara uliolenga kuwashukuru wananchi kwa kukipigia kura chama cha CUF katika uchaguzi mkuu mwaka jana japo hazikutosha.

Rashid alisema kuwa mwaka 1995 serikali ya mapinduzi ya Zanzibar iliwakamata na kuwafunga jela mkiaka 3 watu 18 akiwemo yeye kama mbunge kwa kutoa kauli ya kuipinga serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika kikao cha baraza la wawakilishi .

“Mimi hapa Hamad Rashid mwaka 1995 nilikamatwa na kufungwa jela miaka mitatu na wenzangu 17 kwa kosa la uhaini kwa kutoa kauli za kuipinga serikali i.liyokuwepo madarakani tena ndani ya kikao cha baraza la wawakilishi ….ila tulikamatwa na kufungwa jela…ila leo hawa wenzetu Chadema waapita maeneo mbali mbali ya nchi a kuhamasisha maandamano ya kumkataa Rais Kikwete bila serikali kuwashughulikia viongozi hao”

Alisema kuwa tatizo la vijana wengi ambao wanashabikia hali hiyo ni wale ambao wanafuata mikumbo na baadhi yao kutokuwa na elimu ya kutosha pasipo kutambua kuwa kuipinga serikali iliyopo madarakani ni sawa na uhaini ni kuwa kuendelea kufaya hivyo ni kosa na wanaweza kukamatwa a kufungwa jela.

“Nawaombeni sana wananchi wa mkoa wa Tanga na watanzaia kwa ujumla jiepusheni na maandamano na mikutano inayoandaliwa kwa ajili ya kupinga serikali halali iliyopo madarakani “

Hata hivyo alisema kuwa watanzania wanapaswa kutoendelea kuunga mkono kauli za ubaguzi na uchochezi dhidi ya serikali zinazofanywa na Chadema na kuwa kimsingi tume ya uchaguzi ikimtangaza mshindi na kuapishwa wagombea wote wanapaswa kumuunga mkono na kumtambua kama Rais na kuanza mchakato wa kujipanga na uchaguzi mwingine baada ya miaka mkitano na sio vinginevyo.

“Rais Jakaya Kikwete ndiye Rais wa Tanzania na hakuna sababu ya watanzania kuendelea kudanganywa na wana Chadema kuwa si Rais na kushiriki maandamano na mikutano ya kichochezi inayoendelea kufanywa nchi nzima na chama hicho bila serikali kuchukua hatua”

Pia Rashid alisema kuwa Chadema ni chama ambacho kimekuwa kikiendeshwa na misingi ya ubinafsi wa viongozi wake wasio kubali matokeo na kuendelea kuvuruga amani ya nchi na kukiita CUF ni CCM B maneno ambayo ni ya kitoto kutolewa na viongozi kama hawa wa chadema ambao wanatambua vema katiba ya Taifa na misingi ya vyama vingi.

Alisema kuwa upo utaratibu wa kidemokrasia wa kuiondoa CCM madarakani ukiwemo wa wananchi kujiunga na vyama vya siasa na wakati wa uchaguzi kukichagua chama chao ili kuipokea nchi serikali ya CCM na sio kuhamasisha kuichukia serikali yao.

Hata hivyo aliwataka waunge wa Chadema kutumia bunge kuipinga serikali na sio kwenda kwa wananchi kuhamasisha wananchi kuichukia serikali yao .

Kwa upande wake mwenyekiti wa CUF Taifa Prof .Lipumba katika hotuba yake alisema kuwa uchaguzi mkuu huu ulitawaliwa na uchakachuaji wa matokeo japo kwa upande wao CUF imepata kuongeza idadi ya madiwani na kuwa kwa jiji la Tanga pekee madiwani wameongezeka kutoka 5 mwaka 2005 hadi 9 mwaka 2010 jambo ambalo ni la kuwashukuru wananachi .

Prof. Lipumba alisema kuwa kwa sasa kila mtanzani amepigika kwa ugumu wa maisha kutokana na sela ya kilimo kugeuzwa siasa na seriali ya CCM .

Alisema kuwa misamiati ya kilimo imekuwa ikigeuzwa kila kipindi na kuwa awali ilikuwa ni azimio ya siasa ni kilimo ila sasa ni Kilimo kwanza ila bado watanzania wanamaisha bomu .

Prof Lipumba alihoji Taifa kuendelea kukosa umeme wakati nchi inauwezo wa kuzalisha megawati 500 ila bado nchi imeendelea kuwa nyuma kwa tatizo ,la umeme ,pia yapo makaa ya mawe yenye uwezo wa kuzalisha umeme ila bado Taifa limeendelea kuwa gizani kutokana na ukosefu wa umeme kwa miaka 50 baada ya kujitawala.

Alisema kuwa katika hotuba ya Rais 2006 alidai kuwa mabwawa yamekauka na kuwa kuna mipango yakupata umeme ila 2010 bado kauli ni hiyo hiyo kutokana na kukosa viongozi wazuri wa kumsaidia katika kutatua suala hilo.

Hata hivyo alisema kuwa mkoa wa Tanga ulipaswa kuwa ni mkoa wa kiuchumia nchini kutokana na kuwa na bandari kama kiunganishi cha nchi mbali mbali duniani ila bado mkoa huo upo nyuma tofauti na miji mingine yenye bandari.

“Tunahitaji mabadiliko makubwa yatakayo iwezesha Tanzania kupiga hatua sio kama ilivyo Tanzania ….hivi leo hapa Tanga tunaambiwa kuwa mkuu wa mkoa huu anafanya kazi ya unyang’anyi kwa kupokonya samaki wa wananchi wake kwa kisingizio cha kusafisha mji..hivi mnataka kusema mkoa hauna bwana afya hadi mkuu wa mkoa kufanya kazi ya bwana afya” alihoji Prof.Lipumba

Hata hivyo Prof Lipumba alisema kuwa mwaka 2005 bungeni CUF ndio iliyounda kambi ya upinzani bungeni kwa kushirikisha wabunge wa vyama vingine ila sasa Chadema imekuwa na wabunge wengi na kuunda kambi yake bungeni kwa kuwabagua CUF na vyama vingine.

“Hivi tunawauliza swali viongozi wa Chadema ambao wanatutenga leo wakati sisi tulifanya tamasha la pamoja la kuunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ila leo wanatugeuka na kusema hii ni ndoa ya CCM na CUF nasema haya ni matusi kwa wazanzibar“

Prof Lipumba alisema kuwa mwalimu alionya kuepuka kuwatenga wazanzibar kuwa inaweza kufanya ubaguzi kwa Taifa japo CCM wameelewa hilo na kuepusha ubaguzi ila Chadema wao wanaendekeza ubaguzi na hata kutuita CUF ni CCM B.

“Ndugu zangu huu kusema ni CCM B ni wizi na njama za mwizi ambapo mtu akisema kwa mwizi kwasauti ndogo kuwa mwizi mhusika hupaza sauti zaidi ili kukwepa kupigwa….ukweli Chadema ni gamba la CCM na ndio maana viogogo wanachangia Chadema ili kuanzisha CCM B”

Prof. Lipumba alisema kuwa chama kinachowagawa watanzania hakiwezi kupambana na ufisaji wala kuwakomboa watanzania na kuwa Chadema ni chama kinachotumiwa na wafanyabiashara kwa ajili ya kuficha uozo

"