Adverts

Mar 12, 2011

DARAJA LA KAMSAMBA -SUMBAWANGA VIPI? MH NAKUMBUKA KWENYE ZIARA ULITAMKA NENO!!

MWENYEKITI WA JAMII YA KAMSAMBA AMBAYE PIA NI MCHUNGAJI WAKATI AKIWASILISHA MATATIZO YA WANANCHI WA KAMSAMBA KWA MH RAIS ALIPOFIKA KAMSAMBA NA KUPOKELEWA NA UMATI MKUBWA WA WANACHI WA HAPO, KWA UJUMLA WANANCHI WALIMWOMBA SERIKALI YAKE IJENGE DARAJA LA KUUNGANISHA KILIMATUNDU NA KAMSAMBA HIVYO KURAHISISHA USAFIRISHAJI WA BIDHAA, KUOKOA MAISHA YA WANANCHI KWENYE MTO MOMBA UNAOPITA NA KUTENGANISHA MAENEO HAYO/MIKOA YA MBEYA NA RUKWA





MENEJA TANROADS MKOA WA MBEYA AKIPONGEZWA NA MH RAIS BAADA YA KUAHIDI KUWA TARATIBU ZA MAANDALIZI ZITAANZA MAPEMA KUFANYA UTAFITI JUU YA UWEZEKANO WA KUJENGA DARAJA KATIKA ENEO HILO, JIBU AMBALO LILIONYESHA MATUMAINI KWA WANANCHI KUWA UJENZI WA DARAJA HILO UTAFANYIKA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO YA UTAWALA WAKE -WANANCHI WA KAMSAMBA WANA MATUMAINI BADO KWAKUWA NI MWAKA MMOJA TU TANGU UINGIE MADARAKANI!!
HILI NDILO ENEO LA LINALOTARAJIWA KUJENGWA DARAJA LENYE UREFU WA ZAIDI YA MITA 500 NA HAPA WANANCHI WANAPITA HUKU WAKIPISHANA NA MAMBA KAMA SAMAKI , MWAKA HUU 2011 MTU MMOJA ALILIWA NA MAMBA KATIKA KIJIJI CHA KAMSAMBA MWEZI JANUARY 2011