Adverts

Mar 20, 2011

loliondo kwa babu updates: mvua yatibua mambo, magari yashindwa kwenda, foleni kilometa 30, nauli kwenda kwa babu zapaa!

Hali imezidi kuwa tete baada ya mvua kubwa kujaza mito ya Loliondo
Na Woinde Shizzza wa Globu ya Jamii, Loliondo
Magari ambayo yalikuwa yanaenda kwa Mchungaji Ambilikile Mwsapile 'Babu' katika kijiji cha Samange wilayani Ngorongoro jana yamekwama njiani na kushindwa kuendelea kwenda kutokana na mito kujaa maji kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha. Mkuu wa wilaya ya Monduli Mh. Eliasi Wawalali ameiambia Globu ya Jamii kuwa magari mengi ambayo yalikuwa yanapeleka watu kwa Babu yamekwama baada ya mito ambayo ipo njiani kujaa, hali iliyosababisha magari hayo kusubiri kwa muda mrefu. 'Mito ilijaa kutokana na hii mvua ambayo inaendelea kunyesha hali linayosababish magari kushidwa kuvuka mpaka maji hayo yakapungua.
'Uzuri hjuku kwetu maji yanapungua haraka sana maana mito yetu inapitisha maji mengi na yanawahi kupungua ndo kitu cha kushukuru hicho maana yangekuwa hayapungui sijui ingekuwaje'alisema Mh. Wawalali. Aliongeza kuwa kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo watu wanazidi kufurika na mpaka leo kulikuwa na watu wengi haijawai kutoka ambapo magari yalikuwa yamejipanga kwa urefu wa takriban kilometa 30. Alisema kuwa watu ambao wanapitia barabara ya Mto wa Mbu wamekuwa wakielewa na wamepungua kwa kiasi fulani lakini tatizo ni watu ambao wanatoka kanda ya ziwa kwani wao ndio wanaonekana kuingia kwa kasi kubwa sana. Alisema kuwa anapenda kuwaomba viongozi wa sehemu hizo kutoa elimu kwa wananchi wao ili kuweza kupunguza mkusanyiko kwanza wa watu ambao wapo loliondo ndio wao waje. 'Unajua tatizo la watu sisi tukiwaambia wakae watulie kwanza wasije hawatuamini. Sijui niseme hawatuelewi maana tunaimba kila siku watu ni wengi subirini wapungue lakini hawaamini kabisa.
'Sisi tunawaomba wakae wasubiri watu wakipungua tutawaambia maana huku wanakuja kuteseka tu na jinsi mvua zinavyonyesha watateseka sana. Hivyo wangoje watu ambao tupo huku tutawaambia na watu wanaotoka huku wawaambie wenzao hali halisi'alisema Mh. Wawalali. Kwa upande wake Mchungaji Ambikile Mwasapile alisema kuwa yeye anapenda kuwahudumia watu wote ila kilio chake kikubwa ni kwa wale watu ambao wanawaleta wagonjwa wao wakiwa mahututi.
'Jamani napenda kuhudumia kila mtu ila watu wasilete wagonjwa wao wakiwa mahututi kwani huku wakiwaleta mpaka wafikie kupata huduma ni kazi; hali ambayo inasabaisha wagonjwa wengi wanaoletwa hivyo kufariki 'aliasa Babvu.
Babu ameongezea kuwa katika kijiji cha Samange hakuna watu wa huduma ya kwanza wala hospitali hali inayosabaisha watu ambao wanapelekwa na dripu zao zikiisha hukosa huduma na vifaa vya huduma ya kwanza hivyo wasubiri wapate nafuu ndo wawalete. Hata ivyo katika kituo cha mabasi ya Loliondo kilichopo jijini Arusha kumekuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu wanaoelekea kwa Babu na pia nauli zimekuwa zikipanda siku hadi siku.
Kwas sasa nauli za mabasi ambazo kwa kipindi cha mwisho ilikuwa ni shilingi 60,000/- hadi kufikia shilingi 100, 000/- na kwa yale magari ya Land Cruiser ambayo ilikuwa ni shilingi120,000 kufikia shilingi 150, 000 hali inayosababisha watu ambao hawana uwezo kushidwa kwenda. Globu ya Jamii ilizungumza na abiria mmoja katika kituo cha mabasi ya Loliondo jijini Arusha Bw. Meshaki Alex ambaye alisema kuwa wao kama abiria wamekuwa wakipata shida sana ya usafiri kwani nauli zimepanda kila siku, akaiomba serikali ifuatilie swala hili la nauli ili kila mtu mwenye uwezo na asio na uwezo aweze kwenda kwa Babu kupata kikombe.
"