Adverts

Mar 18, 2011

MBWA MWENYE KICHAA ATESA TUNDUMA

Jioni hii nikiwa katika mji wa Tunduma nimeshuhudia watoto wanne wakikimbizwa kituo cha afya cha Tunduma kutokana na kujeruhiwa kwa kuumwa na mbwa mwenye kichaa.
Mbwa huyo ambaye bado hajakamatwa, ameanza zoezi hilo saa Tisa jioni ambapo inaelezwa kuwa kila anayekutana naye mbele basi humkimbiza na kumg'ata na kisha kutokomea.
Kuna dalili kuwa usiku wa leo mpaka kwisha kwake kutakuwa na matukio zaidi ya kumi ya watu kung'atwa na mbwa huyo ikiwa hakudhibitiwa.
wakizungumza kwenye kituo cha afya baadhi ya wazazi wa watoto waliong'atwa wameeleza kuwa mbwa huyo ametoa ulimi nje wakati wote ambapo anaonekana kutokwa na udenda huku macho yake yakiwa mekundu.