Adverts

Mar 4, 2011

MKUTANO KATI YA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO NA UJUMBE WA WANAWAKE WA MSUMBIJI

Na Hassan I. mabuye- Afisa Habari, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mheshimiwa Sofia Simba (Mb) tarehe 04 Machi 2011, alikutana na ujumbe wa Umoja wa Wanawake wa Msumbiji ulioongozwa na Balozi wa Msumbiji hapa nchini Mheshimiwa Amour Zacarias na Bibi Caterina Pajume ambaye ni mwakilishi katika Tume ya Hifadhi ya Chakula nchini Msumbiji.

Ujumbe huo umekuja na mwaliko kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kupata wajumbe wanawake watakao hudhuria Mkutao Mkuu wa Tatu wa Umoja wa Wanawake wa Msumbiji ambao utafanyika tarehe 26- 30 Aprili, 2011. Bibi Pajume pia aliwasilisha salaam maalum za Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Msumbiji kwa Mheshimiwa Sofia Simba (Mb) kwa niaba ya Wanawake wote wa Tanzania.

Ujumbe huu umeletwa hapa Tanzania tarehe 04 Machi; ambapo tarehe kama hiyo mwaka 1967 ni siku ambayo wanawake wapiganaji wa Msumbiji waliunda umoja wao katika harakati za kudai uhuru na hivyo kutoa mchango mkubwa wa ukombozi wa wananchi wa Msumiji na kudhihirisha kwamba wanawake siyo viumbe dhaifu wasiyo na machango thabiti katika jamii na taifa kwa ujumla.

Mkutano huo wenye lengo la kuwaunganisha wanawake wa nchi ya Tanzania na Msumbiji unafanyika katika kipindi ambacho Msumbiji inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu wa kitaifa; hivyo ni fursa pekee ya kuwahamasisha wanawake waweze kushiriki uchaguzi katika ngazi mbalimbali za maamuzi na uwakilish kwa maslahi ya wananchi wote wa Msumbiji.

Katika mkutano huo Tanzania itawaikilishwa na wajumbe watatu kutoka Tanzania Bara na Visiwani ambao watajumuika katika Mkutano huo wa siku tano nchini Msumbiji. Ushirikano huu unaendeleza jitihada mbalimbli za ushirikiano wa kihisotia uliojengeka tangu kipindi cha kudai uhuru ambapo Tanzania ilitoa mchango mkubwa katika ukombozi wa nchi mbalimbali za kusini mwa Afrika ikiwemo Msumbiji.

Katika kupokea salaam za ujumbe wa Bi. Pajume ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Kilimo nchini Msumbiji, Mheshimiwa Sofia Simba (Mb) alieleza bayana kuwa, Tanzania na Msumbiji ni wamoja kwa nasaba, historia na changamoto zilizopo zinafanana. Ushirikano uliopo unaendelezwa katika ngazi ya familia na kitaifa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu likiwemo daraja linalounganisha nchi ya Tanzania na Msumbiji; daraja ambalo limekuwa kichocheo cha uchumi na maendeleo ya nchi zetu.
"