Ukiwa mdadisi, utafikapo ktk mageti ya kuingia/kutokea ktk hifadhi za taifa unaweza kuona dish kama unalo liona ktk picha hii. Haya ni madish ambayo yanatumika kuunganisha vituo na mageti ya kuingilia kwenye hifadhi ktk mtandao wa komputya wa TANAPA. kupitia mtandao huu, mgeni anaweza kufanya malipo kwa kutumia kadi za taasisi mbalimbali za fedha - za hapa nchini na hata zile za kimataifa. Hizi ni baadhi ya jitihada za kuwapunguzia wageni adha ya kutembea na pesa za kulipia viingilio ktk vivutio vyetu hapa nchini.
Hii ilikuwa ni kwenye geti la kuingilia hifadhi ya taifa ya Tarangire
"