Adverts

Mar 3, 2011

Shy-Rose Bhanji Azawadia Timu Za Netiboli Zilizoingia Daraja la Kwanza

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Shy-Rose Bhanji ametoa jumla ya sh. milioni 1.1 kwa ajili ya kuwapatia mshindi wa kwanza hadi wanne, wa Ligi ya daraja la pili ya netiboli, iliyomalizika mwezi uliopita mjini Morogoro. Timu zilizopata ni mshindi wa kwanza Mbeya sh. (500,000), Mshindi wa pili Polisi Arusha (Sh. 300,000),Mshindi wa tatu, Polisi Pwani (sh. 200,000) na JKT Ruvu iliyopata sh. 100,000 kwa kushika nafasi ya nne. Pichani, Shy Rose, akimkabidhi fedha hizo, Mwenyekiti wa CHANETA Taifa, Anna Bayi, Mjini Dar es Salaam, LEO
"