Adverts

Mar 10, 2011

TANZANIA NA MALAWI KUENDELEZA BONDE LA MTO SONGWE

Waziri wa Maji Pro.Mark Mwandosya akisaini makubalianno hayo huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Umwagiliaji na Maendeleo ya Maji ya Malawi Bwana Sandram Maweru (kulia) akishuhudia Waziri wa Maji Mh Mark Mwandosya (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Umwagiliaji na Maendeleo ya Maji ya Malawi Bwana Sandram Maweru wakibadilishana nyaraka za Makubaliano ya Programu ya Maendeleo ya Bonde la Mto Songwe baada ya kusainiwa katika Hoteli SunBird Mzuzu, Malawi. Prof. Mwandosya akishauriana na wataalamu wake kabla ya mkutano Ujumbe wa Tanzania Mkutanoni hapo

Picha na habari na mdau Nurdin Ndimbe

akiwa Mzuzu, Malawi

Serikali za Tanzania na Malawi zimetiliana saini ya Makubaliano ya Kuendeleza bonde la mto Songwe kwa faida ya Nchi hizo mbili.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mktaba huo na Malawi mwanzoni mwa wiki Waziri wa Maji Pro. Mark Mwandosya alisema kuwa, mkataba wa programu ya Maendeleo ya Bonde la mto Songwe ni muhimu na wa kihistoria na aliishukuru Serikali ya Malawi kwa kuitisha na kugharamia mkutano huo.

Mkutano wetu huu umekuwa ukisubiriwa kwa muda wa siku nyingi kwa Serikali zote mbili, hivyo ni mategemeo yetu sasa makubaliano haya yataanza kutekeleza miradi yote iliyopangwa” alisema. Serikali ya Tanzania na Malawi inasimamia kwa pamoja Progaramu ya Uendelezaji wa Bode la mto Songwe tangu mwaka 2001.

Programu hiyo imegawanyika katika awamu tatu ikiwemo uchunguzi wa awali wa Bonde lenyewe, michoro ya kina ya Bonde pamoja na usimamizi wa miradi iliyotambuliwa ya ujenzi wa mabwawa, usimamizi wa rasilimali ya mto Songwe, uzalishaji wa umeme wa Maji na ujenzi wa miundomindu yake

Waziri Mwandosya alisema pia kuwa, kukamilika kwa makubalino hayo yatawezesha kwa sasa Mamlaka ya Bonde la mto Sonwge kupata mkopo nafuu kutoka Benki ya Maendele ya Africa (ADB) ili kugharamia miradi mbalimbali ya mandeleo katika Bonde hio. “Selikali yangu yangu imepokea taarifa hii kwa furaha kubwa” alisistiza.

Kabla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Kamati ya wataalamu kutoka Tanzania na Malawi ilipitia kwa pamoja rasimu ya makubaliano hayo. Kusainiwa kwa makubaliano hayo pia kutawezesha kisheria kuwa na Mamlaka itakayokuwa na kazi ya kuratibu Programu ya Maendeleo ya Miradi mabalimbali ya Bonde hilo Kwa upande wa Tanzania, pamoja na Wataalamu toka Wizara ya Maji ilijumuisha pia wawakilishi toka Wizara ya Mambo ya Nje,Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Wizara ya Ardhi,Fedha, Madini na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI.

"