Adverts

Mar 22, 2011

TRA WATUHUMIWA KUSABABISHA VIFO VYA WAFANYABIASHARA MBEYA

 Washiriki wa semina iliyoandaliwa na Kituo cha uwekezaji wakisikiliza baadhi ya mada zilizotolewa juu ya kutumia fursa za cheti cha uwekezaji
 Meneja wa TIC kanda ya nyanda za juu kusini Daudi Riganda akizungumzia tatizo la mamlaka ya mapato kusababisha wafanyabiashara kuhama mji wa mbeya na wengine kujiua, wakati wengi kati yao kukumbwa na ugonjwa wa BP kutokana na kubanwa na watu wa TRA kuwanyanyasa hivyo kukwamisha uwekezaji mkoani humo. Kulingana na maelezo yake tofauti na mikoa mingine, mkoa wa mbeya kiuwekezaji umekuwa nyuma kwakuwa wengi wa wafanyabiashara wamekimbia na kuhamia mikoa mingine!!
ofisa mwandamizi  TRA elimu kwa umma  bwana Frank Mkwe akijibu tuhuma hizo ambapo alisema kimsingi kuna mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika kuboresha huduma za mamlaka hiyo na kwamba suala hilo kwa kuwa ni zito ameomba kituo cha TIC wakutane na TRA mkoa ili wayazungumze na kutafuta njia bora zaidi ya kuhudumia wananchi kwani si vyema tuhuma kama hizo zikaachwa hivi hivi kwani mchango wa walipa kodi katika kufikisha malengo ya mkoa unategemea mashirikiano baina ya walipa kodi na mamlaka.