Na Danny Tweve
Dar es salaam
Utafiti uliofanywa na mradi wa Tunaweza /UWEZO kwa wilaya 38 nchini unaonyesha kuwa wanawake wana uwezo mkubwa katika kusoma, kuhesabu na kuandika ikilinganishwa na wanaume.
Katika matokeo ya utagfiti huo uliofanywa mwaka jana inaonyesha kuwa wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ilifanya vizuri ikilinganishwa na wilaya zingine zilizoshiriki kwenye utafiti huo ambapo wilaya ya mwisho ilikuwa Muleba
Utafiti huo ni sehemu ya mradi wa miaka mine unaotekelezwa katika nchi za afrika mashariki katika kufanya tathmini ya uwezo wa watoto wa umri wa miaka 5 hadi 16 katika kusoma, kuandika na kufanya hesabu.
Katika maeneo hayo ya msingi katika upimaji, mwanafunzi katika masomo ya Kiswahili anapaswa kusoma silabi, kusoma maneno, kusoma aya na hatimaye kiwango cha juu kabisa ni kusoma hadithi, wakati kwa somo la kingereza inafanana na kiswahli na hesabu anaanza kwa kutambua namba zilizoandikwa, anafanya hesabu za kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya.
Katika utafiti huo wilaya ya Rombo wanafunzi walioweza kusoma vyema Kiswahili ni 63.8, English 44.5, Hesabu 50.6 ikifuatiwa na wilaya ya Mbulu,Ilemela, Moshi manispaa na Moshi vijijini . katika kundi la pili wilaya zilizofuatia ni Babati, Chunya, Njombe, Mbeya Mjini na Kisarawe.
Kundi la Mkiani ni Muleba ikifuatiwa na Kasulu, Mwanga,Shinyanga vijijini na Liwale.
Utafiti huo kwa mwaka 2011 umepanuka kutoka wilaya 38 hadi kufikia 133 za Tanzania bara ambapo unatarajiwa kufanywa mwezi may ingawa maandalizi yake yameanza tangu 09 march 2011.
Kwa mujibu wa mratibu wa mradi huo Dr Grace Soko matokeo yake ni shirikishi kwa sababu mzazi sanapata mrejesho pale pale wakati watafiti wakiendelea na hojaji kwakuwa watoto na wazazi wanakuwa pamoja nyumbani wakati wa hojaji.