Adverts

Apr 16, 2011

Mama Salma Kikwete Azindua Mradi Wa Maji Hospital Ya Wilaya Mkuranga; Kaya 300 Kufaidika

Mke wa rais Mama Salma Kikwete akisoma risala yake, wakati alipozindua mradi wa maji katika mji wa Mkuranga, katika picha kutoka kulia ni Richard Wells Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), na katikati ni Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adam Malima.
Mke wa rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells, wakati alipowasili katika uzinduzi wa mtambo wa kusukuma maji katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga na kaya zaidi ya 300, Mradi huo umegharimiwa na kampuni ya Serengeti Breweriers kwa kiasi cha shilingi milioni 384.6 na umezinduliwa leo.
Katika picha katikati mwenye miwani ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti (SBL) Teddy Mapunda, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi Nampesya na kulia ni Dr. Florence Temu wa (AMREF)
Mama Salma Kikwete katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Mkuranga na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), kulia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga Adam Malima, Mkurugenzi wa Serengeti Richard Wells, kushoto ni Dr. Florence Temu wa AMREF na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga B. Nampesya.
Mstari wa nyuma kutoka kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano SBL, Brenda Mbathi Mkurugenzi wa Mahusiano (SBL) na mwisho kushoto ni Nandi Mwiyombela Meneja wa kinywaji cha Tusker.