Adverts

May 25, 2011

BREACKING NEWS: AFISA MIPANGO CHAMWINO AJIPIGA RISASI NA KUFA

Marehem Fredy Kaombwe enzi za uhai wake
Ni maskitiko makubwa kwa wadau hasa waliopitia Chuo cha Mipango, mtakumbuka kijana FREDY KAOMBWE aliyehitimu 2006 na baaaye kufanya kazi Halmashauri ya Bahi na baadaye CHAMWINO amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kujipiga risasi.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa licha ya jitihada za kumkimbiza hospitalini zilizofanywa na rafiki na jamaa, roho yake tayari ilikuwa imeshatwaliwa.
Chanzo cha kujiua bado hakijajulikana lakini kuna taarifa zinazohusisha matatizo ya kifamilia.
Kaombwe ambaye ni msomi wa elimu ya Uchumi wa Utandawazi katika ngazi ya Shahada ya pili  ama ya uzamili aliyoipata huko Seoul Korea na kurejea nchini mwaka 2011 atakumbukwa kwa jinsi alivyokuwa mchangiaji mzuri katika kuiona TANZANIA ikipiga hatua za kasi katika maendeleo kwenye mijadala mbalimbali iliyohusisha wanataaluma wa mipango.
Mungu ailaze roho ya marehemu pema amina!