Hili ndilo basi la Sumry likifunikwa na wafanyakazi wa Sumry fasta fasta baada ya kuona timu ya wandishi wa habari ikisogea eneo la Tukio |
ASKARI WA usalama barabarani akikagua sehemu ya mabaki ya basi hilo baada ya kunyofoka kwa front excel |
Na Danny Tweve -Mbeya
Hatimaye takwimu sahihi za vifo vya abiria katika ajali ya basi la Sumry iliyotokea jana usiku mpakani wa Iringa na Mbeya imefikia watu 13 na siyo 15 kama ilivyoripotiwa hapo awali na mtandao huu.
Akizungumza na wanahabari mchana huu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema mpaka sasa maiti 13 wamepokelewa katika hospitali ya rufaa wazazi ya Meta ambako kwa sasa wamehifadhiwa kutokana na kuwepo kwa vifaa vya kutunzia maiti.
Mpaka sasa maiti zilizotambuliwa ni pamoja na Dereva wa Basi hilo Makame Juma, Abiria Frolence Kitaule ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Ubaruku-Mbarali, Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe Thomas Mchalo, ingawa pia taarifa zaidi zinaonyesha kondakta wa basi hilo pia amefariki kutokana na sare za basi la sumry alizovaa ambazo maiti yake imekutwa nazo.