Adverts

May 7, 2011

PINDA BOYS WAIPINDISHA TEMEKE 2-0

Ligi ya Taifa  imeanza jana kwa timu za mikoa ya Nyanda za juu kusini kuanza vyema michuano hiyo baada ya Mbeya wenyeji kuwachapa Iringa 2-0, wakati ambapo pia Pinda Boys wakitoka kifua mbele kwa kuwapindisha Temeke watoto wa Mjini TMK bao 2-1 katika mchezo mkali uliofanyika uwanja wa sokoine.
Pinda Boys walisherekea ushindi huo baada ya kuonyesha wazi kuwa walikuwa wamewasoma vilivyo TMK hasa kipindi cha Pili kwa kuwaendesha mchaka mchaka hadi kupata bao la pili kwa mbinu za kiwango cha juu baada ya mfungaji wao kuzuga kama vile anakwenda kufunga lakini akasita hali ambayo ilimfanya kipa wa TMK kuuzika kirahisi na kuachia lango na hatimaye kupishana na kombora lililoenda nyavuni moja kwa  moja.
Kwa kuwa blog hii huambatana na picha indaba africa inakuletea sehemu matukio ya mechi hiyo.

Kasoro ndogo ndogo hazikosi kujitokeza kwenye michezo hapa score board ikiwa haionyeshi nani kapata nini, ni dalili za maandalizi ya ligi ya Taifa kutokuwa katika viwango tarajiwa, ama wenyeji wamejisahau- hapa ni katika uwanja wa sokoine wakati wa mechi ya Pinda boys Vs Temeke TMK


Ujumbe wa mwalimu Nyerere ukisomeka kwenye paa la uwanja wa sokoine kuwa maendeleo  ya nchi  maskini, hayawezi kupatikana kwa msingi wa Fedha, bali........................... watu wanafuatilia mchezo kati ya TMK na Pinda Boys


Dogo huyo alitishia kama vile anapiga shuti golikipa akatishika then akaachia kombora la akili lililoenda wavuni huku wachezaji wa TMK wenye nyeupe wakishangaa, hilo lilikuwa goli la pili lililowapa ushindi Pinda Boys na kutoka kifua mbele kwa 2-1


Mlinda Mlango wa Pinda Boys akitoka uwanjani kwa furaha huku akikumbatiwa na mshabiki baada ya kuwezesha timu yao kutoka ikiwa imeacha burudani ya ushindi

Dua ni muhimu baada ya ushindi, ndivyo walivyotekeeleza vijana wa Pinda jana baada ya ushindi dhidi ya watoto wa Mujini TMK

Mchezaji Bora kwa mechi ya Temeke na Pinda Boys Sundey Hindu akipokea zawadi ya shilingi 100,000 kutoka kwa mgeni rasmi wa mchezo huo baada ya kuiwezesha timu hiyo kutoka kwa ushindi mtamu, tayari ameonekana kuanza kuwaniwa na baadhi ya timu zilizotuma mawakala kufuatilia uchezaji wa wachezaji wa mikoani katika ligi hiyo ya taifa picha zote kwa hisani ya Indaba africa.