Ilikuwa siku ya Jumanne ya tarehe 26/04/2011. nilikuwa naelekea Dar es salaam baada ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka. nikiwa nimekaa kiti cha nne kutoka kwa dereva wa basi la Sumry. kama ilivyo kawaida ya abiria wakifika katika eneo hilo lenye mteremko wenye kona kani abiria walipunguza uhuru wao wa kuongea na walioendelea walizungumza kwa sauti ya chini. Mara baada ya dakika tano hivi nikasikia sauti kutoka upande wa dereva; " ona hao, hao, huyo huyo anaovatake Fuso, hawa jamaa wana roho ngumu" abiria tukaanza kuhangaika kuangalia kinachotokea mbele, ndipo nikaona wapanda baiskeli wawili wakiwa wafunga vyombo vya plastiki (madumu) kwenye vibebeshi vya baiskeli zao wakishuka mteremko kwa kasi. kondakta akasema " hawa jamaa huwa wanafunga matawi ya miti chini ya viatu vyao ( kata mbuga) ili kupunguza msuguano na lami kwani hawatumii kabisa breki za baiskeli zao, kufika mwisho na matawi yanakuwa yamekwisha sagika kabisa". abiria mmoja aliyekuwa nyuma ya dereva ambaye alionekana kuwa ana uzoefu wa maeneo hayo alidakia na kusema " mwaka jana kuna gari la mizigo lilifyatuka breki na kuacha njia na kupinduka, kesho yake wakati wafuatilia vifaa vya gari bondeni walikuta maiti ya mtu imeoza na pembeni kidogo waliona baiskeli na madumu matatu ambayo yalisadikika kuwa yalikuwa na ulanzi kwani nyasi za maeneo hayo zilikuwa zimeungua" kondakta akaendeleza soga na kusema " ukienda vilabu vya vijijini Iringa utaona maeneo ya haja ndogo nyasi zimeungua kama zimepigwa na gramaksoni" abiria walichek sana. Ilikuwa ni vigumu kuwapita wajasilia mali hao kwa sababu walikuwa kati kati ya barabara mpaka tulipofikia eneo la mwisho wa mteremko ndipo basi likawapita.
Mwanavuli