Adverts

Jun 1, 2011

BREACKING NEWS; ABOOD BUS LAPINDUKA MLIMA NYOKA MBEYA



Taarifa tulizopata jioni hii ni kwamba basi la Abood lililokuwa limetokea jijini Dar kuja Mbeya limepinduka katika mlima nyoka nje kidogo ya jiji la Mbeya.
Hakuna aliyepoteza maisha kutokana na tukio hilo ingawa kuna taarifa za majerahI kadhaa huku wengine wakipata majeraha  madogo madogo kutokana na abiria kusukumana wakati wa  kujiokoa.
Taarifa zinadokeza kuwa jumla ya abiria 31 walifikishwa usiku huu hospitali ya rufaa ya Mbeya ambako wamepata matibabu na wengi kuruhusiwa ingawa hali ya dereva ni mbaya.
Inadaiwa kuwa gari hilo limegongana na fuso wakati wakipishana na gari jingine ambapo lilitanua njia na kusababisha dereva wa abood kutafuta njia ya kuokoa abiria wake na kujikuta akiparamia upande mwingine ambao gari lilipinduka lakini akafanikiwa kuokoa abiria wake kwakuwa eneo hilo ni hatari kutokana na mteremko uliopo endapo angeamua kukutana uso kwa uso na roli hilo.