Wakazi wa nchini Uingereza usiku wa kuamkia leo walipata fursa ya
kuona kupatwa kwa mwezi ambapo mwezi huo ulionekana"mwekundu kama damu" kwa
takriban dakika 100. Hata hivyo, wanasayansi wa taasisi ya mambo ya anga ya
Marekani (NASA) walieleza kuwa
wakazi wa Ulaya hakufaidi vizuri tukio hilo kwani ulionekana kabla ya mwezi
kuchomoza kulingana na ya huko nchi za
Ulaya)
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kupitia mtandao wa
barua pepe tukio hilo lilianza saa 12 na dakika 24 jioni kwa muda wa majira ya
joto ya nchini Uingereza (1824 British Summer Time) na kuendelea
hadi saa 6 usiku (0000 BST) lakini kwa Uingereza ulianza kuonekana saa 3 na
dakika 19 usiku (2119 BST).
Aidha wakazi wa maeneo ya nusu ya mashariki
ya bara la Afrika, eneo la Mashariki ya Kati, Asia ya Kati na magharibi mwa
Australia pia waliweza kuliona
tukio zima kwa takribani dakika 100 za kupatwa kwa mwezi. Hata hivyo, wakazi wa
Marekani hawatoliona tukio hilo kwa vile litatokea majira ya mchana kwa nyakati
hizo.
Kijiografia, asili ya mwanga wa mwezi ni mionzi ya jua. Tukio la
kupatwa kwa mwezi ni pale Dunia, Jua na Mwezi zinapokuwa mstari mmoja, na kivuli
cha Dunia kinaangukia kwenye Mwezi kamili. Uwekundu kama damu katika tukio hilo
la leo ni matokeo ya miale ya jua kupita Duniani kisha kuangukia kwenye uso wa
mwezi…(Rashid Mkwinda kwa Msaada wa vyanzo mbalimbali vya habari |