Askari wa FFU wakiwa wametapakaa mtaani kutuliza vurugu ambapo ameelezea hali ilivyotokea kwa Machinga kukaidi kuondoa katika eneo lilozuiliwa na halmashauri ya jiji kutumika kwa biashara. Vurugu hizo zimetokana na makundi ya vijana vibaka na wala sio Machinga ambao wamehamasika na kuanza vurugu kwa Kuvunja nyumba za biashara, kuvunja madirisha ya nyumba, kuchoma magari moto, kupora mali za watu, ambapo pia majeruhi watatu wamelazwa hospitali ya bugando.
Kandoro amesema, hivi sasa kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na yeye, imekutana katika kikao cha dharura na tayari uchunguzi umeanza ili kujua chanzo cha vurugu hizo, zinazo sadikiwa kuchochewa na wanasiasa, lakini pia watu walijeruhiwa, mali ziliharibika ikiwa ni pamoja na thamani ya vitu vilivyoharibiwa katika vurugu hizo.
Machings hao, inasemekana wamegoma kwenda katika eneo walilopangiwa la kiloleli, mlango mmoja na miti mirefu ambako wangefanya biashara zao na kuondoka katikati ya jiji.
Vijana hao wakiliangusha gari walichome moto...
gari jingine likiteketea kwa moto...
Picha kwa hisani ya http://thebigtopten.blogspot.com/
"