Jul 8, 2011
MELI YA KUTAFITI MAFUTA,GESI MAFIA NA , MTWARA HII HAPA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa pili kulia) na mkewe Tunu wakiwa katika mzungumzo na viongozi waandamizi walioshiriki katika uzinduzi wa mali ya kufanyia utafiti wa mafuta na gesi katika pwani ya Mtwara na Mafia kabla ya uzinduzi uliofanywa na Mama Tunu Pinda katika mji maarufu wa uundaji meli wa Geoje, nchini Korea Kusini. (PICHA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiongozwa kukagua meli ya Ocean Rig Poseidon baada ya kuizindua kwenye bandari ya Mji maarufu kwa ujenzi wa Meli kubwa wa Geoje nchini Korea ya Kusini Julai 8, 2011. Meli hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Petrobas ya Brazil inatarajiwa kufanya utafiti wa mafuta na gesi kwenye pwani ya mtwara na Mafia miezi michache ijayo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizindua meli ya Ocean Rig Poseidon kwenye bandari ya Geoje nchini Korea ya Kusini Julai 8, 2011. Meli hiyo mali ya kampuni ya Petrobas ya Brazil inatrajiwa kuwasili nchini miezi michache ijayo ili kufanya utafiti wa mafuta katika Pwani ya Mtwara na Mafia. (Picha na Ofisi ya Waziri MKuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua meli ya Ocean Rig Poseidon baada ya meli hiyo kuzinduliwa na Mama Tunu Pinda kwenye Bandari maarufu kwa ujenzi wa meli kubwa ya Mji wa Geoje nchini Korea Kusini Julai 8, 2011. Meli hiyo mali ya Kampuni ya Petrobas ya Brazil inatarajiwa kufanya utafiti wa mafuta na gesi kwenye pwani ya Mtwara na Mafia miezi michache ijayo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akihutubia baada ya kuzindua meli ya Ocean Rig Poseidon kwenye bandari ya Geoje nchini Korea ya Kusini Julai 8, 2011. Meli hiyo mali ya kampuni ya Petrobas ya Brazil inatrajiwa kuwasili nchini miezi michache ijayo ili kufanya utafiti wa mafuta katika Pwani ya Mtwara na Mafia. (Picha na Ofisi ya Waziri MKuu)
"