Adverts

Jul 9, 2011

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA JIJINI MBEYA LAPAGAWISHA MASHABIKI, YAANI WANAJISIKIA MAJOTROO TU

Mwendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta tayari umepamba moto katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, ambapo wasanii mbalimbali tayari wameshapanda jukwaani huku wengine wakijiandaa kufanya mambo makubwa katika jukwaa la Serengeti Fiesta jioni hii, Hapa anaonekana mwimbaji wa muziki wa Hiphop Prof. Jay akiimba nyimbo zake, kama vilee piga makofi katika tamasha hilo llililovutia watu wengi. Watu wengi wanaonekana kuwa wenye furaha na wanaojisikia Majotroo kwelikweli katika tamasha hilo linalodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti SBL, kwani wamekuwa na mzuka wa kweli wakati wotw wa tamasha hilo
Profesa Jay akiimba na mmoja wa mashabiki wake aliyemuita jukwaani ili kumpa tafu katika moja ya nyimbo zake.
Mashabiki wakinyanyua mikono yao juu kuashiria kukubali muziki uliokuwa ukiporomoshwa na wasanii wa tamasha la Serengeti Fiesta jijini Mbeya jioni hii.
Hapa wakiimbishwa vilivyo na msanii wa muziki wa Hiphop MwanaFA aka Binamu
MwanaFA akiimbisha mashabiki wake katika tamasha la Serengeti Fiesta uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jioni hii.
Hapa katika picha msanii Belle9 anaonekana akipagawisha mashabiki wake jukwaani kwa nyimbo zake nzuri zinazopendwa na mashabiki wake.
Msanii Top See akiimba katika tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika kwenye uwanja wa Sokoine jioni hii.
Jafarai naye amepata nafasi ya kuwaambia mashabiki wake kwa wimbo wake wa Watu Kibao hapa uwanjani.
Ulinzi umeimarishwa kama unavyoona watu wa usalama wakiwa wamejipanga kila mahali ili kuhakikisha usalama wa mashabiki pamoja na wasanii.
Rais wa Masharobaro akiruka juujuu jukwaani wakati akifanya vitu vyake.
Rais wa Masharobaro na kundi lake wakionyesha uwezo wao mbele ya mashabiki wao.
Umati Mkubwa umefurika uwanjani hapo na watu wanaendelea kuingia uwanjani ili kushuhudia tamasha la Serengeti Fiesta.
"