Jul 23, 2011
WAZIRI MUNDU ATUA MBEYA, ATETA NA MKUU WA MKOA KWA SAA1.15
Waziri wa Uchukuzi Omary Nundu amewasili mkoani mbeya akiwa na ujumbe wa watu wanne akiwemo kiongozi wa chama cha wasafirishaji wa mizigo Zacharia Hans Pope kwa lengo la kushughulikia mgomo wa madereva wa magari yanayopeleka mizigo nje ya nchi.
Waziri huyo ambaye awali alipanga kuzungumza na madereva hao majira ya saa 10, kwa matarajio ya kuwasili saa 9.00 alasiri alichelewa na kutua uwanjani mbeya majira ya saa 1.40 Usiku.
Mara baada ya kuwasili alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya ambapo aliungana na kamati ya Ulinzi na usalama akiwa yeye na ujumbe wake ambapo waliteta kwa takribani saa 1.15 juu ya mgogoro huo.
Imeelezwa kuwa mkutano huo utafanyika asubuhi majira ya saa tatu katika eneo la Sogea mjini Tunduma.
Indaba africa kama kawaida itaendelea kuwapa kila kinachojiri kuhusiana na suala hilo, ambalo kwa namna moja limeathri uchumi wa nchi, huku hali ya uchafuzi wa mazingira katika mji wa Tunduma ikiendelea kushika kasi kutokana na msongamano wa magari ambao umepelekea hata huduma za jamii kupungua eneo la Vyoo .