Adverts

Aug 23, 2011

ASKOFU MKUU WA KKKT ALEX MALASUSA APOKEWA KWA SHANGWE MBOZI

Maaskofu wa KKKT kuanzia kushoto DrHans Mwakabana wa KKKT dayosisi ya kusini Kati Bulongwa, Askofu Shayo wa KKKT -Kilimanjaro, Dr Alex Malasusa Askofu Mkuu KKT Tanzania na Askofu Dr Israel Mwakyolile wa Dayosisi ya KONDE wakiwa katika UKUMBI wa Moshi  hotel mjini Vwawa.

Maaskofu pamoja na wachunngajhi na viongozi wengine wa usharika wa Vwawa na jimbo la Magharibi Mbozi.

Askofu Malasusa akipokea mkeka kutoka kwa askofu Mwakyolile kama zawadi ya waumini wa jimbo la Magharibi Mbozi

Dereva wa askofu Mkuu akipokea zawadi , hatua hii ilipokelewa kwa furaha na askofu mkuu na kueleza kuwa madereva wamekuwa wakisahauliwa, licha ya kazi nzito wanayoifanya katika kutunza maisha yao.

Askofu Malasusa akielezea jambo kuhusiana na askofu Shayo ambaye aliongozana naye huko sumbawanga kwaajili ya huduma ya misioni Mpya iliyoanzishwa huko.

Kimunya Frank Kilasi pamoja na Mama walikuwepo kwenye hafla hiyo

Askofu Shayo na Askofu Mwakyolile wakifurahia jambo baada ya kukabidhiana zawadi ya Jamvi ama mkeka

Kumbe hata kwenye dini kuna nyimbo za solidarity forever eeeeh nimezoea kusikia kwenye mei mosi wanapoimba wafanyakazi lakini jana usiku ilikuwa kama hivi

Askofu Dr Hans Mwakabana akipokea mkeka kutoka kwa Dr Mwakyolile ambaye ni askofu wa dayosisi ya Konde

Picha na kwaya ya Vwawa usharikani

Mzee Moshi akisalimiana na askofu Mkuu KKKT Dr Alex Malasusa katikati ni mama moshi baada ya kuandaa chakula cha jioni kwa viongozi hao waliokuwa safarini kutoka sumbawanga.

Moshi na Mkewe wakiwa kwenye picha ya pamoja na maaskofu Dr Shayo na Dr Malasusa

Maaskofu na viongozi aw jimbo la Mbozi Magharibi

Askofu Mwakyolile akisiliza jambo huku anayefuatia kulia ni Mchungaji Mwaipopo  Askofu Msaidizi  anayeshilia dayosisi la Dodoma akifuatiwa na mchungaji Mwakihaba naibu askofu wa dayosisi ya Konde