MABONDIA Asha Abubakar na Fadhila Adam wanatarajia kudundana katika
pambano la kuhamasisha ngumi kwa wanawake litakalofanyika siku ya Idd
pili katika uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.
Pambano hilo litakuwa ni miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika
pambano la marudiano kati ya mabondia wa ngumi za kulipwa Fransic Cheka
na Mada Maugo.
Pambano hilo la ubingwa wa UBO linatarajia kuwa katika raundi 10 uzito
wa Kg 72 huku likisimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa (PST).
Akizungumza Dar es Salaam jana, Promota wa ngumi hizo Kaike Siraju
alisema, pambano hilo la kuhamasisha litakuwa la raundi 6 huku likiwa
katika uzito wa kg 52 ambalo litakuwa ni moja ya pambano la kivutio
siku hiyo.
"Wanawake ni wachache sana wanaoshiriki katika mchezo huu hivyo ni
naimani watu watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wadada hao,"
alisema kaike.
Alisema, kwa upande wa Maugo na Cheka kila bondia anaendelea kujifua
katika gym yake tayari kwa kusubiri siku hiyo ambapo maandalizi
yanaendelea.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na huzwaji wa DVD zenye
mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth,
Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya
juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha maarufu Rajabu
Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' hapo hapo uwanjani na kwa Dar es Salaam
DVD hizo zinapatikana katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi
--