Adverts

Aug 24, 2011

taswa yaunda kamati kuratibu tamasha la michezo kuadhimisha miaka 50 ya uhuru

TASWA imeunda Kamati ya Watu 16 kwa ajili ya kusimamia masuala ya tamasha la wanamichezo kwa ajili ya miaka 50 ya Uhuru.
Kamati hiyo itaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Uhariri ya gazeti la Raia Mwema, Johnson Mbwambo, ambaye amepata kuwa Mhariri wa Habari za Michezo wa magazeti mbalimbali nchini na pia ni miongoni mwa waasisi wa TASWA.
Pia TASWA imemteua Mhariri Mkuu wa gazeti la SpotiStarehe, Masood Sanani kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Sanani ni Mhariri mzoefu, ambapo pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Tuzo za Wanamichezo Tanzania inayoandaliwa na TASWA, ambayo Mei mwaka huu ilifanya kazi kubwa kuandaa tuzo za aina yake.
Pia wapo Wajumbe wa Kamati hiyo ya Tamasha la Miaka 50 ya Uhuru, ambao ni wahariri wa siku nyingi na wana uzoefu mkubwa na masuala ya michezo na waandishi wa michezo, wajumbe hao ni Said Salim ambaye licha ya kuwa mhariri veteran pia ni mwalimu wa waandishi wa habari, ambapo anaishi Zanzibar, jambo litakalosaidia pia kuhusishwa wanamichezo wa zamani wa Zanzibar.
Mwingine ni Mhariri wa gazeti la ThisDay, Willy Chiwango, ambaye pia mkongwe katika masuala ya taaluma ya habari na mwenye uelewa mkubwa wa mambo ya michezo.
Wajumbe wengine ni:
1. Asha Muhaji-Mhariri Leap Media
2. Rashid Zahoro- Mhariri gazeti la Burudani
3. George John-Katibu Msaidizi TASWA
4. Mahmoud Zubeiry- Mhariri Dimba
5. Mohammed Mkangara-Mhazini Msaidizi TASWA
6. Juliana Yassoda-Naibu Mkurugenzi Idara ya Michezo
7. Majuto Omary-Mwenyekiti TASWA FC
8. Ephraim Kibonde- Mtangazaji Clouds FM
9. Deo Rweyunga-Mkurugenzi Radio One
10. Chacha Maginga-Mtangazaji TBC1
11. Amour Hassan-Mhariri Nipashe
12. Zena Chande-TASWA
Chama cha Gofu Wanawake Tanzania (TLGU).
Katibu wa Kamati atakuwa George John Katibu Msaidizi wa TASWA. Kamati itafanya kikao chake cha kwanza Jumapili Septemba 4, 2011.
(D) Semina ya waandishi Morogoro
Maandalizi yanaendelea kuhusiana na semina kwa waandishi wa habari itakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao mkoani Morogoro na ile itakayofanyika Oktoba mkoani Arusha, ambazo tunaamini zitakuwa za manufaa kwa wadau wetu.