Adverts

Oct 25, 2011

furaha sumalu aongelea channel 127 ya DSTV

furaha sumalu aongelea channel 127 ya DSTV:
Kwa takribani miezi minne sasa,watanzania na watu wote wanaoongea au kutumia lugha ya Kiswahili wamekuwa wakiburudika na kuelimika kupitia channel mpya kabisa ndani ya DSTV inayokwenda kwa jina Africa Magic Swahili inayopatikana katika namba 127.
Hivyo hutokosea ukiamua kuiita Channel 127 ya DSTV.Kama bado hujapata fursa ya kutazama Channel 127,nakushauri ufanye hivyo leo hii. Nini kilipelekea kuanzishwa kwa Channel hiyo ambayo kila kukicha inazidi kujipatia umaarufu?
Inawasaidiaje wasanii wa tasnia ya filamu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati katika kutimiza malengo yao na kupanua soko lao?Je,utaratibu wa kuingiza filamu yako katika Channel hiyo kama wewe ni muundaaji,muongozaji au msanii wa filamu ukoje?
Ili kupata majibu kwa maswali hayo na mengineyo,nilimtafuta Meneja Masoko wa DSTV-Tanzania,Furaha Samalu(pichani). Huko mbele kuna maswali niliyomuuliza na majibu kutoka kwake.