Baba mzazi wa kijana huyo juu akiwa chini ya ulinzi wa polisi jamii
Vijana wapiga nondo wakiwa chini ya ulinzi mkali wakati wa msako ulioanza majira ya saa 2 hadi asubuhi eneo la Muungano, Kigamboni ,Frelimo n.k
Vibaka watano wanaodaiwa kuhusika na upigaji nondo wakiwa chini ya ulinzi wa sungusungu
Fedha ambazo wapiganondo hao wamesalimisha baada ya kujeruhi watu wawili majira ya saa 2 eneo Mawele wele mjini Iringa wakati msako ukiendelea
Fedha ambazo wapiganondo hao wamesalimisha baada ya kujeruhi watu wawili majira ya saa 2 eneo Mawele wele mjini Iringa wakati msako ukiendelea
Msako mkali ukifanywa na wananchi wa kata ya Mwangata na Mkwawa leo huku mwanamke mmoja pekee akijitolea kushiriki msako huo
Sakata la wananchi kupigwa nondo katika kata ya Mkwawa na Mwangata Manispaa ya Iringa limeendelea kuchukuasura mpya baada ya wananchi wa kata hizo wakiongozwa na sungusungu na polisi kufanya msako mkali nyumba kwa nyumba na kufanikiwa kuwakamata washiriki wa mtandao huo zaidi ya wanne pamoja na mali mbali mbali ambazo wananchi walipokonywa.
Sakata la wananchi kupigwa nondo katika kata ya Mkwawa na Mwangata Manispaa ya Iringa limeendelea kuchukuasura mpya baada ya wananchi wa kata hizo wakiongozwa na sungusungu na polisi kufanya msako mkali nyumba kwa nyumba na kufanikiwa kuwakamata washiriki wa mtandao huo zaidi ya wanne pamoja na mali mbali mbali ambazo wananchi walipokonywa.
Pamoja na msako huo kufanyika katika nyumba za wananchi hao pia mmoja kati ya vibaka amekutwa ndani ya chuo cha kanisa la Anglikana eneo la Mawele wele akiwa amefichwa na mzazi wake.
Pia kijana mmoja kati ya waliokamatwa katika msako huo ni mtoto wa mchungaji wa kanisa moja la kilokole mjini Iringa ambaye amekamatwa maeneo ya Muungano .
katika msako huo vijana hao walikuwa wakipokea kipigo kikali kutoka kwa wananchi hao wenye hasira kali na baada ya hapo vijana hao wamekuwa wakitaja orodha ya matukio na idadi ya watu ambao wamewapiga nondo na kutaja pia kushiriki kumuua kijana Damas Kisinga .
Vibaka hao ambao majina yao tunayo japo kwa sasa yamewekwa kapuni kwaq muda ili kuendeleza msako zaidi wapo wanafunzi ,mtoto wa askari mstaafu wa jeshi , mtoto wa mchungaji wa kilokole na wote ni vijana kati ya miaka 20 hadi 35 na kuwa kila wanapopiga mtu nondo mali hukabidhi wa wakubwa wao na wapo hupata mgao wa kati ya shilingi 5000 hadi 20000 kwa makusanyo yanayozidi kiasi cha shilingi 200,000.
Wamedai kuwa baadhi yao wamekuwa wakilazimishwa na viongozi wao hao kushiriki katika vitendo hivyo ,ambapo viongozi hao wao wamekuwa wakitoa maelekezo ya watu wa kuwavamia na wale wa kupigwa nondo hadi kufa ama kukatwa mapanga.
Wamedai kuwa hadi sasa kuna orodha ya nyumba zaidi ya 50 katika manispaa ya Iringa ambazo zilikuwa katika mpango wao wa kwenda kuzivamia na kufanya uporaji .
Hata hivyo walidai kuwa walikuwa katika maandalizi ya kufanya uporaji mkubwa katika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa na kuwa mtandao wao kwa sasa ni mkubwa zaidi.
Pia alisema kuwa mtandao huo umeendelea kukua zaidi baada ya kukamatwa na kuachiwa na polisi na kuwa baadhi ya washiriki wa mtandao huo ni wale waliopata kutumikia vifungo jela na baadhi ya wamekuwa wakikamatwa na kuachiwa na polisi .
Wakati kipigo kikali kikiendelea kwa vibaka hao mmoja kati yao amesalimisha fedha kwa sungusungu hao kwa madai kuwa fedha hizo kiasi cha zaidi ya shilingi 20,000 kuwa walikuwa wametoka kupora usiku wa leo.
Wakati huo huo wananchi wamelitaka jeshi la polisi mkoani Iringa kutoa waachia mapema watuhumiwa hao wa upigaji nondo na kuhoji sababu ya mmoja kati ya watuhumiwa aliyekamatwa juzi ambaye ni mzazi wa Msafiri Ilomo kuachiwa huru kabla ya upelelezi wa suala hilo kukamilika .
Msaka huo bado unaendelea usiku huu na mimi nitaendelea kuwapa taarifa kulingana na matukio yatakavyo jitokeza