Adverts

Nov 20, 2011

Mzee Nterege: Miaka 103 ana watoto 57, wajukuu 200, vitukuu 70

Diwani na mzee Nterege Nyigana Mutari ana umri wa miaka 103,
*AMEOA WANAWAKE SITA, AMEJENGA SHULE YA KUSOMEA FAMILIA YAKE
Na Renatus Masuguliko KWA mara ya kwanza niliposikia habari za mzee Nterege Nyigana Mutari ana umri wa miaka 103, ana watoto 57, wajukuu 200 na vitukuu 70, sikuamini. Nilijiuliza maswali mengi moja likiwa ni kwa nini mzee huyo asiwemo katika kitabu cha maajabu ya dunia? Hiki ni kitabu ambacho huchapishwa kila mwaka kikiwa na mkusanyiko wa rekodi za dunia kuhusu mafanikio ya binadamu pamoja na maajabu mbalimbali. Kuishi miaka 103 na kuwa na watoto 57 sio jambo dogo, watoto ambao nao wanakuletea wajukuu 200, na wajukuu nao wanakuletea vitukuu 70.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea Hapa.....>>>>>>