Adverts

Nov 30, 2011

Waziri wa mambo ya nje Kenya apingana na uamuzi mahakama kuu!kulikoni?

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya ameelezea wasi wasi wake mkubwa katika maamuzi ya mahakama kuu ya kuamuru kukamatwa kwa rais wa Sudan Omar al Bashir.
Kwa mujibu wa VOA Mosses Wetangula alisema katika taarifa jumanne kuwa amri hiyo haisaidii kitu na inasababisha msuguano wa moja kwa moja juu ya msimamo wa kwamba wakuu wa nchi hawawezi kushitakiwa kwa mashitaka ya uhalifu. Ameongeza kuwa serikali ya Kenya inatafakari juu ya kukata rufaa.
Rais Al Bashir anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa mashitaka ya uhalifu wa kivita katika eneo la Darfur Sudan ambapo serikali yake imekuwa ikipambana na waasi tangu 2003.
Hivi karibuni Mahakama kuu ya Kenya ilitoa uamuzi kwamba serikali ya nchi hiyo lazima imkamate Bashir kama akiingiza mguu wake” nchini humo. Lakini Waziri wa mambo ya nje anapopinga hilo serikali inatoa picha gani tunageukia maneno ya mwimbaji aitwaye Jaguar na kusema hili si kigeugeu?!!! Habari hii kwa hisani ya sundauSumari
Sikiliza katuni ya wimbo huo ukiongozwa na Raila!