Adverts

Dec 9, 2011

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL, MGENI RASMI MKESHA WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU MNAZI MMOJA DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kuwahutubia wananchi waliohudhuria mkesha wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck sadick, akizungumza jukwaani kutoa salam za sherehe hizo kwa wananchi.
Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Wasanii wa Kundi la Safi wakiwapagawisha wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Wanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma, wakiimba jukwaani ikiwa ni sehemu ya kutoa burudani maalum ya kusherehekea sherehi hizo.
Rapa na mwimbaji wa Bendi ya TOT Plus, Jua Kali, akighani rap zake jukwaani wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
Wanenguaji wa Bendi ya Msondo Ngoma, wakishambulia jukwaa wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha JKT Mgulani, wakishambulia jukwaa kwa kucheza ngoma ya Bugobogobo ya Kabila la Wasukuma, wakati wa sherehe hizo.
Mbunge, John Shibuda, akipagawishwa na ngoma ya Kisukuma ya Bugobogobo, iliyokuwa ikipigwa na wasanii wa kundi la JKT Mgulani.
Wasanii wa Kundi la Taarab la Culture kutoka Zanzibar, wakitoa burudani jukwani.
Wasanii wa kundi la Sanaa la Safi Theatre, wakimpagawisha Mbunge Msindai, jukwaani wakati wakishambulia jukwaa.
Wasanii wa Kundi la Safi wakiwapagawisha wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Kapten John Komba, akiongoza kundi lake la Kwaya kuimba wimbo maalum wa Maadhimisho ya Sherehe hizo jukwaani.
Wasanii wa Kundi la Sanaa la Safi Theatre, wakionyesha umahiri wao jukwaani wa kucheza Sarakasi.
Baadhi ya Wabunge na wananchi wakimtunza Kaptein John Komba wakati akiimba jukwaani.
HATIMAYE ULIFIKA MUDA WA KUANZA RASMI SHAMBRASHAMBRA ZA MAFATAKI.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyesha Rimoti kufyatua Mafataki ikiwa ni sehemu ya kuzindua rasmi Mkesha wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 Uhuru zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja usiku wa kuamkia leo. Kutoka (kushoto) ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal na (kulia) ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova, baada ya kuzindua rasmi sherehe hizo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. KUTOKA KWA SUFIAN MAFOTO