Adverts

Dec 8, 2011

picha za sherehe ya uhuru zinaongea zenyewe kabla ya siku yenyewe..

Vifaa vya Kivita vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vikiwa katika mazoezi ya maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana. Sherehe hizo zinafikia Kilele cheke kesho ambapo shughuli zote zitafanyika katika Uwanja huo wa Uhuru ambapo sherehe za mkesha wa sherehe hizo zitaanza leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mgeni rasmi akiwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Magari ya Kivita na Vifaa vya kivita yakipita mbele ya jukwaa Kuu wakati wa mazoezi ya Wanajwtz. Kila aina ya gari la Kivita lilipita wakati wa mazoezi hayo. Vijana wa Scout wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya sherehe hiyo kwenye Uwanja huo huo wa Uhuru. Mazoezi yanaendelea uwanjani hapo. Ni mazoezi ya vijana hao Chipukizi wakijifua na mazoezi ya silaha. Kesho ndo utakuwa mziki mnene.mia