Adverts

Dec 11, 2011

TANZANIA YAONGOZA KATIKA STADI ZA ELIMU AFRIKA MASHARIKI

TANZANIA imekuwa kileleni mwa nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika kwa kasi ya ukuaji sekta ya elimu, imeeleza ripoti maalumu iliyotolewa hivi karibuni
Katika ripoti hiyo, iliyotolea na shirikisho maalumu la taasisi zinazosimamia elimu katika ukanda huo, Kenya imeshika nafasi ya pili katika somo la Hisabati, baada ya Mauritius.
Ingawa zimekuwa vinara katika somo hilo, kwa mujibu wa Shirikisho la Kufuatilia Ubora wa Kitaaluma katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, Tanzania inaongoza kwa ujumla hasa kwenye stadi za usomaji, ikifuatiwa na Shelisheli, Mauritius na Swaziland.
Shirikisho hilo linahusisha wafuatiliaji wa pamoja kutoka katika Wizara za Elimu na Mabaraza ya Mitihani ya nchi 15 zilizoshirikishwa katika utafiti huo. Nchi zilizobaki katika ukanda huo wa Afrika Mashariki na Kusini zikiwemo Malawi, Zambia, Lesotho, Namibia na Uganda, kwa mujibu wa matokeo hayo zimeripotiwa kufanya vibaya hasa katika somo la Hisabati, baada ya kubainika kwamba wanafunzi hawawezi hata kukokotoa matatizo kwa kutumia kanuni ya msingi kwenye somo hilo.
Shirikisho hilo limetoa taarifa hiyo iliyoiinua Tanzania, baada ya kufanya utafiti kwa kuhojiana na wanafunzi 4,436 wa darasa la sita kama sampuli kwenye shule 193 katika nchi husika. Nchi za Malawi, Zambia, Lesotho, Msumbiji na Uganda, zimeripotiwa pia kufanya vibaya zaidi katika suala la stadi za usomaji.
“Viwango vya ubora wa elimu katika nchi 15 bado ni duni japokuwa kumekuwa na jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na serikali za ukanda huu kwa ajili ya kuboresha viwango hivyo,” alisema mkuu huyo wa shirikisho hilo, Demus Makuwa. Utafiti huo ulijumuisha majaribio ya somo la Hisabati kwa wanafunzi hao kwenye nchi hizo 15.
Shirikisho hilo linahusisha mtandao maalumu wa Wizara za Elimu kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya kielimu na malengo ya maendeleo ya milenia. MAONI YANGU : TAFAKARI CHUKUA HATUA!!!!