Adverts

Dec 9, 2011

Wakuu wa Nchi mbali mbali walipokuwa wakiwasili nchini kwa ajili ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Rais wa Bunge la Korea Mhe. Kim Jong Nam akupita kwenye gwaride la heshima kwenye Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es salaam wakati alipowasili nchini jana. Mhe. Kim Jong Nam ameambatana na ujumbe wa watu 17 akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea, kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Mhe. Kim Jong Nam, Rais wa Bunge la Korea wakiangalia vikundi vya Burudani mara baada ya kuwasili nchini. Mhe. Nam amepokelewa pia na Mhe. Selina Kombani, Waziri wa Katiba na Sheria (kulia).
Waziri Membe, akimtambulisha Rais wa Malawi Mhe. Bingu wa Mutharika, kwa viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili mjini Dar es salaam jana. Rais Mutharika amepokelewa pia na Mhe. Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Kilimo wa Tanzania. Rais Bingu wa Mutharika amefuatana na ujumbe wa watu 15 kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara hapo kesho tarehe 9.12.2011.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akimtambulisha Rais wa Msumbiji Mhe. Armando Guebuza kwa Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi Mhe. Mathayo David Mathayo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. KUTOKA MICHUZI BLOG