TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAHUSIANO MABAYA SANA KATI Y A TFF NA AFRICAN LYON FC
Kwa masikitiko makubwa sana, uongozi wa timu ya African Lyon Fc inapenda kuwaeleza watanzania hususani wapenzi wa mpira wa miguu kuwa, katika jitihada zote za timu yetu ya kukuza na kuedeleza soka hapa nchini, Tumekuwa na mahusiani MABAYA SANA na chama cha mpira wa miguu yaani TFF. Napenda kuweka wazi bila kificho chochote kuwa TFF imekua ikitukandamiza na kutuchafua mbele ya jamii kwa makusudi. Tena ni kana kwamba si mtu mmoja ndani ya TFF bali ni kuwa agenda ya TFF nzima. Kuanzia kwa Rais wa shirikisho kamati ya mtendaji, kamati ndogondogo na pia sekretarieti cha kusikitisha kama si kufurahisha mpaka kwa walinzi wa milangoni siku za mechi. Napenda nitoe baadhi ya mifano michache ambayo tunakutana nayo katika jitihada zao za kutuyumbisha pamoja na vilio vyetu vya kila siku. RATIBA YA LIGI KUU. Timu zote ambazo zimekua zikienda kucheza mechi kanda ya ziwa zimekuwa zikicheza mechi zote mbili(yaani kucheza na Toto Fc na Kagera sugar). Kitu ambacho African Lyon Fc chini ya uongozi wetu hatujawahi kukutana nacho. Nakama hiyo haitoshi mechi yetu ya mwisho wanatupeleka Manungu Turiani kucheza dhidi ya JKT Ruvu na hali sisi na JKT uwanja wetu ni Chamazi alafu wenyeji wa Turiani (mwenye Uwanja wao) Mtibwa wanapelekwa Morogoro kucheza dhidi ya Moro United. Ni vigezo vipi vilivyowekwa kutupeleka sisi na si Simba wala Yanga. Je hii TFF ni ya Simba na Yanga tu.- MBWANA SAMATA
- YUSUFU SOKA
TFF kupitia kwa kaimu Katibu mkuu wake bwana Sunday Kayuni na wakala waliamua kumpeleka Sweden mtaja hapo juu na tunasikia kuwa hivi sasa yupo Jela. Tunalaani na tunaomba vyombo vya dola viingilie kati na sheria ichukue mkondo wake vielelezo vya mchezaji alivyoondoka na wahusika wa safari yake tunavyo.
- TIKETI ZA MILIONI 35
Mwaka 2009 TFF walituomba tuwaletee tiketi toka Marekani zenye thamani ya shilingi milioni 40 na wakaturudishia tiketi za shilingi milioni 5 zilizobakia baada ya kutumia katika mechi kadhaa hivyo kwa sasa tunawadi milioni 35. Tiketi zenyewe zilitumiwa kwa mechi mbalimbali zikiwemo za Kilimanjaro Taifa Cup na Kagame cup. TFF wamekuwa mara kwa mara wanatoa ahadi hewa juu ya malipo yetu. Hii inatufanya tuzidi kuamini kuwa TFF haina nia nzuri na timu yetu African Lyon Fc. Tunaomba tulipwe.
- SWALA LA KASSIM DEWJI
TFF nathubutu kusema kuwa haiko makini kwa jambo lolote lile hapa nchini, baada ya sisi kununua timu 2009/2010. Timu yetu ilipata zawadi ya sh.milioni 5 kama timu yenye nidhamu bora cha kushangaza kaimu Katibu mkuu ndugu Sunday Kayuni alimuandikia hundi kwa jina la Kassim Dewji,huku akijuafika kuwa sisi ndio tunaomiliki timu, na hata kama angekuwa yeye ni mmiliki bado jina lingekuwa ni la timu na sio la mtu binafsi.
Kuna uwezekano mkubwa sana hela hizo viongozi wa juu kabisa wamegawana na ndio maana wanalikingia kifua. Tunataka hela zetu, hii ni haki ya wachezaji.Ni nidhamu gani aliyoonyesha uwanjani Kassim Dewji mpaka apewe yeye?
- FEDHA ZA VODACOM 2010 – 2011
Jamani hadi leo hii tumepokea shilingi 3.5 milioni tu. Je wenzetu wote wamepewa hivyo? Vodacom wanajua? Halafu wanataka bado tuvae jezi za Vodacom ambao udhamini wao ni wa hela ya mboga. TFF wanajipaka matope na aibu iwakute kwa wizi wa mchana kweupe.
TAMKO LA AFRICAN LYON
African Lyon Fc kwa nguvu zetu zote na tunapenda tuelewe kuwa TFF ina mpango madhubuti wa kuishusha timu yetu daraja kama si kuiondoa kwenye ramani ya soka.
Hivyo basi tunatoa siku 30 kwa TFF kukutana nasi na kuzungumzia matatizo yetu na kama ikishindikana basi sisi tunajitoa kwenye ligi pasipo kujali chochote.
Asante sana.
Kwa maelezo zaidi wasiliana:Sherally Abdallah Hammed
0759 302496