Zantel ambayo ni kampuni Tanzu ya ya Etisalat Group na ambayo ni kampuni ya simu selula yenye ubunifu mkubwa nchini Tanzania inayofuraha kutangaza kuwa imemteua Bw. Brian Karokola kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Masoko pamoja na Bw. Deo Kwivukwa kuwa Mkuu wa Idara ya Usambazaji na Mauzo kuanzia Januari 02, 2012.
Jukumu jipya la Bw. Karokola kama Mkurugenzi wa Masoko litakuwa ni kusimamia programu ya mikakati ya mipango ya masoko, mawasiliano ya kampuni kwa kuangalia mtiririko wa mapato ya rejareja na kubuni mipango mipya. Nafasi hiyo ni muhimu katika kuendelea kukua kwa bidhaa za Zantel pamoja na soko lake nchini Tanzania.
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Zantel, Ahmed Mokhles akiidhinisha uteuzi huo alisema kwamba Zantel ni mwajiri wa kuchaguliwa na Watanzania na chimbuko la kukuza utaalamu wa ndani.
“Ninayo furaha kuwatangaza uteuzi wa Bw. Karokola kama Mkurugenzi wa Masoko na kuifanya Zantel kuongoza miongoni mwa waendeshaji wa mitandao ya simu selula kwa kuteua mzawa kuongoza kitengo chake cha masoko. Hili lipo kwenye majukumu ya Etisalat Group katika kuwekeza kwenye wataalamu wa ndani”, alisema Mokhles.
Brian Karokola ana Shahada ya Uzamili kwenye Masoko (MBA) na hivi karibuni alimaliza programu ya miezi 12 ya HiPo ambayo inajumuisha programu ya uongozi kibiashara kazini kwenye mawasiliano ya simu inayotolewa kwa ubia kati ya Etisalat Academy kwenye Falme za Kiarabu (UAE) na Skuli ya Biashara ya Harvard ya Marekani.
Deo Kwivukwa kwa upande wake kama Mkuu wa Kitengo na mauzo jukumu lake litakuwa ni kuangalia usambazaji, timu ya mauzo na kusimamia mwenendo wa usambazaji nchini hali kadhalika kuwezesha na kupanua bidhaa za Zantel zisambae nchini kote.
Kabla ya uteuzi wake alikuwa ni msimamizi wa kitengo cha Zantel Own Manager kinachoshughulikia maduka na vituo vya huduma kwa wateja . Ana Shahada ya Uzamili kwenye Masoko akiwa amejikita kwenye masuala yanayoliweka soko kwenye hali mbaya (MBA venturing in Marketing) .