Indaba blog is rural based online news for rural and urban community!!
Adverts
Jan 7, 2012
CHUO CHA MIPANGO DODOMA CHAJIIMARISHA KUTOA HUDUMA ZA USHAURI NA UPANGAJI MIPANGO VIJIJINI
Maafisa Mipango wanaosomea Stashahada ya uzamili katika Mipango ya Mikoa, Miradi, Mazingira na Utawala Bora hivi karibuni walipiga kambi kwa siku kumi katika kijiji cha Wami Dakawa Mkoani Morogoro kusaidiana na wananchi kutengeneza mipango ya maendeleo ya kijiji hicho. Hapa wanachuo hao wakihamisha ramani iliyochorwa ardhini na kuiweka kwenye karatasi tayari kwa kuunganisha kitaalamu kutokana na vipimo vya GPS walivyochukua wakati wa matembezi ya kataa ya njia
Mkufunzi wa chuo hicho Bw Titus Mwageni akisisitiza jambo mbele ya wanakijiji wakati wa utengenezaji wa Mipango hiyo
Hapa ni eneo la shule ya msingi Wami Dakawa ambapo huduma za maji zimekuwa zikitolewa, miongoni mwa changamoto zilizobainishwa ni pamoja na uchangiaji usio wa tija kuwezesha raslimali maji kuwa endelevu kijijini hapo
Choo cha shule ya msingi Wami Dakawa ambacho kimejengwa kwa ufadhiri wa taasisi moja ya kigeni ambacho ni cha mfano kwa jamii ya kijiji hicho katika kuendeleza teknolojia ya uvunaji wa maji ya mvua. Pia kupitia mfumo huo shule itakuwa sasa inatekeleza mpango wa taifa wa usafi (osha mikono) unaolenga kujenga tabia ya usafi mtu atokapo haja ili kuepusha magonjwa ya mlipuko na ya matumbo.