FM ACADEMIA WAWASHA MOTO DAR LIVE MBAGALA

BENDI ya muziki wa dansi nchini ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, usiku wa kuamkia leo walifanya makamuzi ya kufa mtu ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.
Wanamuziki hao pia walisifia mandhari ya ukumbi na jukwaa la muziki na kuahidi watahakikisha wanafanya shoo katika ukumbi huo kila siku ya Alhamisi kutokana na wingi wa mashabiki waliohudhuria.


Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo wakiserebuka.

Mmoja wa waimbaji wa bendi hiyo ‘akigonga’ kongoro ukumbini hapo.


Wanenguaji wote wa bendi hiyo wakiwa kwenye pozi la pamoja


Warembo wakifuatilia shoo hiyo.
Baadhi ya wanenguaji wa kike wa bendi hiyo wakiwa katika pozi.

Rapa Toto Kalala akiwa majukumu yake.